In Summary

• Mwakilishi wadi katika bunge la kaunti ya Kimabu ameaga dunia baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani karibu na shule ya upili ya Mangu.

Image: hisani

Mwakilisji wadi maalum katika bunge la kaunti la Kiambu Ezra Kabuga Kihara ameaga dunia katika ajali ya barabarani mapema Jumapili tarehe 22 Septemba katika barabara ya Thika karibu ya shule ya upili ya Mangu.

Kifo cha MCA Ezra kimedhibitishwa na gavana wa kaunti ya Kiambu mheshimiwa Kimani Wamatangi kupitia timu yake ys mawasiliano.

Aidha kupitia ukurasa wake wa X, gavana Wamatangi amesikitikia kifo cha Ezra akimtaja kama kiongozi kijana mahiri ambaye kujitolea kwake na shauku yake ya kuwatumikia watu wa kaunti ya Kiambu ilidhihirika katika kila kipengele cha kazi yake.

Gavana Kimani Wamatangi amesikitia kumpoteza mbunge mchanga kama Ezra Kabugi.

Gavana Wamatangi amesema kuwa Ezra alijitolea na alikuwa mwenye ahadi nyingi kwa siku zijazo kwa wakaazi wa kaunti ya Kiambu.

Kulingana na walioshihudia kisa hicho kwa asubuhi mwendo wa saa kumi na moja ni kuwa, gari la mwakilishi wadi huyo liligonga lori lililokuwa limeegeshwa.

Gari hilo la Ezra liliwaka moto baada ya kugongana na lori hilo.

 

 

View Comments