In Summary

• Malala amedai kwamba mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohamed na mwenzake wa Homabay Town Peter Kaluma wanatarajiwa kuwasilisha hoja ya kutokuwa na imani na Gachagua.

DP RIGATHI GACHAGUA
Image: DPCS

Wandani wa Naibu Rais Rigathi Gachagua sasa wanashutumu kinara wa upinzani Raila Odinga na chama cha ODM kwa kuchangia malumbano katika muungano wa Kenya Kwanza.

Aliyekuwa katibu Mkuu wa UDA Cleopas Malala amedai kwamba mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohamed na mwenzake wa Homabay Town Peter Kaluma wanatarajiwa kuwasilisha bungeni hoja ya kutokuwa na imani na Gachagua kama naibu wa rais.

Viongozi hao waliokuwa wameandamana na Gachagua siku ya Jumapili walikuwa ni pamoja na Malala, Gathoni wa Muchomba, Karungo Thang'wa na Mejjadonk walionya kuwa iwapo hoja hiyo itawasilishwa bungeni, basi lazima rais Ruto atakuwa ameithinisha mwenyewe.

Naibu Rais Rigathi Gachagua na washirika wake waliendeleza mashambulizi dhidi ya mrengo wa Rais William Ruto, ishara ya kuzorota kwa mshikamano ndani ya himaya ya Kenya Kwanza.

Naibu rais akiwa mjini Thika Jumapili alimuonya rais Ruto kuwa iwapo chama cha UDA hakitawekwa sawa, basi ana hatari ya kupoteza imani ya wenyeji wa Mlima Kenya na kwamba hakuna kitakachofanyika kuokoa hali hiyo.

Gachagua alisema kuwa hakuna atakayemwamini tena Ruto ikiwa ataendelea kuwaruhusu washirika wake kumdhalilisha.

"Ruto alitoa ahadi moja ambayo haihitaji ufadhili wowote, haihitaji IMF au Benki ya Dunia. Aliahidi kuwa chini ya uangalizi wake hatakubali naibu wake kudhalilishwa. Ikiwa hawezi kutimiza ahadi hiyo moja, basi hakuna mambo mengine ambayo watu wanaweza kumwamini," Gachagua alisema.

 

View Comments