In Summary

• Mshukiwa mkuu Irene Auma mwenye umri wa miaka 30 anazuiliwa na polisi akisubiria kufikishwa mahakamani.

• Mshukiwa katika kisa cha Rusinga alifanikiwa kutoroka baada ya bangi kwenye magunia na  mitungi 30 ya chang'aa yenye thamani ya shilingi 240,000 kupatikana.

Image: X//DCIKenya

Maafisa wa upelelezi kutoka kitengo cha kupambana na dawa za kulevya katika kaunti ya Kwale wamewakamata watu wawili na bangi ya thamani ya shilingi 9,241,500.

Wawili hao wamekamatwa kufuatia msako wa maafisa wapolisi katika eneo la Kona ya Chief, Diani kaunti ya Kwale.

Maafisa wa kupambana na dawa za kulevya  walipokea taarifa kuhusu walanguzi hao wawili.

Baada ya kudokezewa kuhusu bidhaa hiyo haramu, polisi walimkamata Hamisi Omar ambaye aliwaelekeza katika ghala ambapo bangi hiyo ilikuwa imewekwa.

Polisi walipata gunia kumi zenye uzani wa kilo 314.05 katika msako huo uliotia mbaroni mshukiwa wa pili kwa jina Irene Auma mwenye umri wa miaka 30.

Wakati huo, polisi kutoka kata ya Rusinga magharibi walinasa magunia mengi ya bangi yenye thamani ya shilingi milioni 1,749.000.

Maafisa wa polisi pia walipata mitungi 30 ya pombe haramu aina ya Chang'aa  yenye thamani ya shilingi laki mbili na elfu arubaini.

Mshukiwa katika kisa cha Rusinga aliyetambuliwa kwa jina Kevin Barasa maarufu kama Kevo alifanikiwa kutoroka.

Hassan Omar na Irene Auma wanazuiliwa na polisi wakati msako wa kumtafuta Kevin Barasa ukiendelea.

Dawa za kulevya zilizopatikana zinazuiliwa na polisi na zitawasilishwa mahakani kama ushahidi.

View Comments