In Summary

•Uchapishaji wa maudhui kama hayo yanakiuka sheria ya udhibiti wa dawa za kulevya ya 2010 na sheria ya udhibiti wa dawa za kulevya na vitu vya kisaikolojia ya 1994.

Mamlaka ya kitaifa ya kupambana na pombe na matumizi ya dawa za kulevya NACADA, imewaonya watengenezaji wa maudhui ya mtandaoni na washawishi dhidi ya kukuza matumizi ya vileo na dawa za kulevya.

Hii ni kupitia kwa barua kwa watengenezaji wa maudhui iliyotiwa sahihi na afisa mkuu mtendaji wa NACADA Dkt. Anthony Omerikwa Jumatatu 23, Septemba.

Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, NACADA imesema kwamba imebainisha kuwa kumekuwepo ongezeko washawishi wa mitandao wanachapisha maudhui yanayolenga kuendeleza utumizi wa dawa za kulevya.

NACADA inasema tabia hiyo inarudisha nyuma juhudi zake za kupigana na matumizi ya vileo na mihadarati katika vijana.

Hata hivyo, mamlaka hiyo imewarai watengeneza maudhui na washawishi wa mitandao kuwacha kutumia majukwaa yao kuhubiri injili ya matumizi ya dawa za kulevya.

NACADA imeonya umma kuwa yeyote atakayepatikana akichapisha maudhui ya yanayokuza matumizi ya dawa za kulevya atakabiliwa na mkono wa sheria.

Kulingana na NACADA ni kuwa, kuchapisha maudhui kama hayo yanakiuka sheria ya udhibiti wa dawa za kulevya ya 2010 na sheria ya udhibiti wa dawa za kulevya na vitu vya kisaikolojia ya 1994.

Aidha mamlaka hiyo imewataka wazazi na walezi kuhakiki kwa ukaribu maudhui ambayo watoto wao wanatazama kwenye mitandao ya kijamii.

View Comments