In Summary

•Kuria asema si sharti mjane arithi kiti kilichokaliwa na bwana

•Kura ya kuamua mridhi kufanyika Mei 18

 

Moses Kuria
Image: FILE

Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria amemkejeli mjane wa aliyekuwa mbunge wa Juja marehemu Francis Waititu almarufu 'Wakapee' , Susan Njeri kwa kumezea mate kiti kilichokuwa cha mumuwe.

Mbunge huyo mwenye utata na mbwe mbwe si haba kwenye ulingo wa siasa amedai kuwa sio lazima  kwa Njeri kukirithi kiti kilichoachwa wazi baada ya kifo cha mumewe mwezi  Februari mwaka huu.

Kupitia akaunti yake ya Facebook, Kuria anayejulikana kuwa mwandani  wa naibu Rais William Ruto aliwataja wajane za waliokuwa watu maarufu ambao hawakuchukuwa nyadhifa zilizowachwa wazi na mabwana zao.

 

"Wachumba wawili wake marehemu John Demathew sio wasanii baada ya bwanao kuaga, mbona mkewe wa marehemu Wakapee afanywe mbunge...

Mkewe mwendazake Wanugu hakubadilika kuwa mwizi baada ya Wanugu kuaga.. Vile vile mkewe hayati Magufuli hakufanywa rais pale Tanzania, mbona huyu wa Wakapee lazima apewe kiti kilichoachwa na bwanake??" Kuria aliandika.

Facebook post - Moses Kuria's post on Facebook
Kuria's Facebook post - Chapisho la Kuria kwenye Facebook.

Waititu alifariki mwezi Februari mwakani baada ya kuugua saratani ya ubongo kwa muda. Kwa sasa kampeni zimenoga sana katika eneo bunge hilo lililo Kaunti ya Kiambu.

Kura ya kuamua nani atakayeridhi kiti hicho inatarajiwa kufanyika tarehe kumi na nane mwezi huu wa Mei. Kinyang'anyiro hicho kimewavutia wagombea kiti wasiopungua 13 akiwemo Susan Njeri ambaye alikuwa mkewe  marehemu Waititu.

Susan anagombea kiti hicho kwa tikiti ya chama tawala cha Jubilee.

Moses Kuria kupitia chama chake cha People Empowerment Party amesimimamisha  George Koimburi.

View Comments