In Summary

•Katika karatasi za mahakama iliyofikia Radio Jambo, mfanyibiashara huyo alisema anatumiwa kama 'kisingizio' kwa kuwa ni raia anayetii sheria.

•Wanawe ambao walikuwa miongoni mwa waliokamatwa, anasema, bado wanashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Pangani.

Nancy Indoveria Kigunzu almaarufu Mathe Wa Ngara katika makao makuu ya DCI baada ya kukamatwa Jumatatu jioni.

Nancy Indoveria Kigunzu, almaarufu Mathe Wa Ngara amesema haelewi ni kwa nini polisi walimtafuta.

Katika karatasi za mahakama iliyofikia Radio Jambo, mfanyibiashara huyo alisema anatumiwa kama 'kisingizio' kwa kuwa ni raia anayetii sheria.

"Sijawahi kufanya uhalifu wowote nchini Kenya wala sijawahi kujihusisha na uhalifu wowote binafsi au kwa kushirikiana na watu wengine na kwa hivyo sielewi ni kwa nini polisi wanatafuta kunikamata," alisema katika karatasi za mahakama zilizowasilishwa na Wakili Shanice Maingi. .

Anataka mahakama itoe amri ya kusimamisha kukamatwa kwake, jambo ambalo tayari limetokea, kushtakiwa mbele ya mahakama bila wapelelezi kufanya uchunguzi, na kumpa fursa ya kusikilizwa.

Nancy pia anaitaka mahakama itoe amri ya kumpa dhamana aliyoitarajia, kwani alifahamu shughuli za watu kukamatwa zilizofanywa Ngara kupitia vyombo vya habari.

“Siku chache baadaye iliripotiwa kwenye vyombo vya habari kuwa mmoja wa watu waliokamatwa ni mtu asiye sahihi, aliyefahamika kwa jina la ‘Mathee wa Ngara’,” anasema.

Aidha, Mathe Wa Ngara ameishutumu Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai na Inspekta Jenerali wa Polisi kwa kutumia ofisi zao kuwakamata na kuwaweka kizuizini wanawe wawili kinyume cha sheria.

Wawili hao ni watoto wenye umri wa miaka 16 na 17 mtawalia.

Alisema anaamini lengo la kukamatwa kwa wanawe linalenga kumtishia na hatimaye kumkamata bila kufuata utaratibu.

Wanawe ambao walikuwa miongoni mwa waliokamatwa, anasema, bado wanashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Pangani.

Wao na wengine wawili walitarajiwa kortini Jumatatu, Agosti 21.

View Comments