Rais wa shirikisho la soka barani afrika  Ahmad Ahmad, ameachiliwa huru nchini  Ufaransa bila kufunguliwa mashtaka yoyote  baada ya kuhojiwa huko Marseille ,mwendesha mashtaka mjini humo amesema .

Xavier Tarabeux  amesema Ahmad,  aliyekuwa nchini Ufaransa kwa mkutano wa  Fifa  uliofanyika siku ya jumatano  alihojiwa katika sehemu ya uchunguzi  kuhusu ufisadi  na ulagjai  wa kughushi stakabadhi .

View Comments