mariga.harambee.stars

Siku ya Jumatano, aliyekuwa kiungo wa Harambee Stars, McDonald Mariga alitembelea kikosi cha timu ya taifa mjini Cairo, Misri kabla ya mechi yao dhidi ya Tanzania.

Baada ya Harambee Stars kupoteza mechi yao ya kwanza katika kipute cha kombe la ubingwa bara Afrika dhidi ya Algeria siku ya Jumapili.

Matokeo hayo yaliwacha timu ya taifa ya Kenya katika hali mbaya kwani itabidi wamepata ushindi dhidi ya Tanzania na pia kulazimisha sare dhidi ya Senegal ili kufuzu katika raundi ya 16 bora.

Akijua kibarua ambacho kitawakumba kikosi cha Stars, Mariga alisafiri hadi Misri ili kuwapa motisha kabla ya mechi hiyo ambayo itakuwa kama fainali.

Katika kanda tuliyo iona, Mariga ambaye ni nduguye nahodha Victor Wanyama, aliwahimiza wachezaji hao kusahau matokeo ya mechi iliyopita na kuweka juhudi zote hii leo.

Akizungumza katika lugha ya sheng, Mariga aliwakumbusha kuwa mechi hii ni kama fainali na wanapaswa kuwacha nguvu zote katika uwanja ili kutoka na ushindi.

"Hiyo game ya Algeria ishapita watu wasahau. Hii game ya Tanzania tu give hard, hii ni finali wasee, tu deadi kwa uwanjo, kama ni mbaya ni mbaya, hii ni finali. Hakuna kitu ingine." Alisema Mariga.

Tazama kanda ifuatayo.

https://twitter.com/MichKatami/status/1143827876434841600

View Comments