- Harambee.Stars.6
- Harambee.Stars.10

Siku ya Jumanne, Julai 2, 2019, Waziri wa michezo, balozi Amina Mohammed, aliwapongeza wachezaji wa Harambee Stars mjini Cairo, Misri kwa juhudi zao katika kipute cha AFCON.

Mohammed ambaye alikuwa ameandamana na balozi wa Kenya nchini Misri, Joff Otieno, aliwapongeza kwa kukazana kisabuni katika mechi zote tatu ambazo walicheza, ingawa hawakufuzu katika raundi ya 16 bora.

“Mlifanya mlifanya kadri ya uwezo wenyu. Na kama jinsi rais alisema wakati mlikuwa katika ikulu, lengo kuu halikuwa ushindi pekee bali nyie kufanya zaidi ya uwezo wenyu, na hilo mlifanya.”  Alitamka waziri Amina Mohamed.

Amina alikuwa anazungumza alipoandalia kikosi hicho cha Stars, karamu ya chakula cha mchana.

“Tuna furaha sana kwa kuwa mlifuzu kufika hapa baada ya miaka 15, na sasa ni wakati kuhakikisha kuwa katika kila  kipute cha AFCON.” Aliongeza Amina.

Rais wa shirikisho la kadanda nchini, Nick Mwendwa, alisisitiza shukran za dhati kwa serikali kwa usaidizi wao wa hali ya juu baada ya timu ya taifa kurudi katika michuano ya bara la Afrika kwa mara ya kwanza kwa miaka 15.

“Sijawahi ona serikali ikitusaidia kama jinsi walivyo tusaidia katika safari hii ya AFCON. Kwa hili tunataka kusema Asante sana." Alisema Mwendwa.

Kenya walishindi mechi moja na kupoteza mbili kati ya tatu katika mechi za kundi C na kushindwa kufuzu katika awamu ya 16 bora.

View Comments