Frank Lampard ameteuliwa meneja mpya wa Chelsea kwa kandarasi ya miaka mitatu. Anachukuwa nafasi ya Maurizio Sarri aliyeondoka mwishoni mwa msimu uliyopita.

Hadi kuteuliwa kwake, Lampard mwenye umri wa miaka 41 alikuwa meneja wa timu ya Derby County.

Alichezea Chelsea kwa kipindi cha miaka 13 kabla ya kuondoka mwaka 2014 na kujiunga na Klabu cha New York City katika ligi ya Marekani.

Akiwa Chelsea alishinda jumla ya mataji 11, yakiwemo matatu ya ligi ya primia na ligi ya mabingwa barani Ulaya mwaka 2012.

Atakuwa na jukumu la kuongoza Chelsea katika kipute cha ligi ya mabingwa msimu ujao mbali na kuimarisha nafasi ya timu hiyo katika ligi ya primia.

View Comments