- walcott (1)
- walcott
- everton 1
- everton

Mshambulizi matata wa Everton na timu ya taifa ya Uingereza, Theo Walcott ni miongoni mwa wachezaji sugu wa Everton ambao wamewasili nchini hii leo, tayari kumenyana na Kariobangi Sharks katika mechi ya kirafiki hapo kesho.

Mchezaji huyo ambaye alijishindia nyoyo za mashabiki wengi haswa kina dada wakti alipokuwa akizitikisa nyavu katika klabu ya Arsenal, alionekana mchangamfu pindi tu ndege ya timu hiyo ilivyotua.

Kikosi hicho cha Marcos Silva kinatumia mechi hii kama mojawapo ya maandalizi kemkem kabla ya msimu mpya ujao.

Everton ilimaliza msimu uliopita ikiwa katika nafasi ya nane ndani ya ligi kuu ya Uingereza baada ya kujizolea alama 54.

The Blues watamenyana na kikosi cha Kariobangi Sharks katika uga wa Kasarani siku ya Jumapili mida ya saa nane mchana. The Toffees wanarejea Afrika Mashariki miaka miwili baada ya kutembea Tanzania ambapo walicheza na Gor Mahia.

Kikosi cha Everton ambacho kimewasili Nairobi:

Maarten Stekelenburg

Jonas Lossl

Mason Holgate

Lewis Gibson

Morgan Schneiderlin

Dennis Adeniran

Tom Davies

Theo Walcott

Ademola Lookman

Leighton Baines

Andre Gomes

Oumar Niasse

Ryan Astley

Callum Connolly

Morgan Feeney

Antonee Robinson

Beni Baningime

Joe Williams

Nathan Broadhead

Fraser Hornby

Josh Bowler

Nathangelo Markelo

View Comments