ighalo

Mabingwa watetezi Cameroon na wenyeji Misri wameyaaga mashindano ya AFCON  baada ya Cameroon kufungwa 3-2 dhidi ya Nigeria jijini Alexandria.

Mabao ya Nigeria yalifungwa na Odion Ighalo wa Shanghai Greenland ambaye alicheka na nyavu mara mbili, huku kiungo wa Arsenali, Alex Iwobi akifunga la ushindi.

Misri nao wamepigwa mbele ya mashabiki elfu sabini jijini Cairo na Afrika Kusini kwa goli moja tu lililofungwa na Thembinkosi Lorch katika dakika ya 85.

Kwingineko, Arsenal huenda ikamsaini winga wa Uhispania Lucas Vazquez, 28, kwa mkataba wa pauni milioni 31 kutoka Real Madrid wiki ijayo.

Leicester inaelekea kuvunja rekodi ya uhamisho wa wachezaji kumsajili kiungo wa kati wa Monaco na Ubelgiji Belgium Youri Tielemans,22, ambaye aliyecheza kwa mkopo, uwanja wa King Power karibu nusu ya msimu uliyopita.

View Comments