Mshambulizi wa harambee stars Michael Olunga pamoja na Nahodha wa harambee stars Victor Wanyama wamewaongoza wakali wa harambee stars kuipa pole familia yake Joe Kadenge.

Joe Kadenge aliaaga dunia siku ya jumapili akiwa katika hospitali kuu ya Nairobi akiwa na umri wa miaka themanini na minne. Wakenya wengi wanamkumbuka Kdenge kwa maqmbo aliyoifanyia timu ya taifa ya stars huku wengi wao wakiwa ni wachezaji wa kikosi cha taifa cha Kenya.

Olunga pamoja na wenzake wa Harambee stars walituma jumbe zao za kumuomboleza Kadenge huku wengi wakimtaja kama kielelezo chema kwao na jamii nzima.

View Comments