Oh No! Wanariadha 2 wa Kenya wapigwa marufuku .
Wanariadha wawili wa Kenya wamepigwa marufuku dhidi ya kushiriki mashindano ya riadha baada ya kupatikana na makosa ya kutumia dawa zilizoharamishwa . Bingwa wa mwaka wa 2014 wa Glasgow Commonwealth na bingwa wa afrika wa mbio za mita 10,000 Joyce Chepkirui na mwanariadha wa masafa marefu John Jacob Kibet Kendagor ndio wakenya hivi punde kupigwa marufuku .
Chepkirui, ambaye pia alishinda mbio za marathon za Amsterdam na Honolulu marathons mwaka wa 2015 kando na kumaliza wa 10 katika Boston marathon mwaka huo amepigw amarufuku Athletes Integrity Unit (AIU) baada ya kasoro kutokea katika vipimoa vya sampuli ya kumtambua yaani Athletes Biological Passport (ABP).
Chepkirui, aliyeshinda medali ya fedha katika mashindano ya ubingwa wa afrika mwaka wa 2011 katika mbio za mita 1500 na fedha tena katika mbio za nyika za afrika mwaka wa 2012 hajashiriki mahsindnao yote mwaka huu .Chepkirui, aliyekulia katika wilaya ya Buret huko Rift valley alianza kukimbia katika ulingo wa kimataifa mwaka wa 2007 katika mashindano ya ubingwa afrika kwa chipukizi ambapo alimaliza wa tano katika mbio za mita 1500.