- PA-32488855
- Maguire2
- Harry-Maguire-714909

Mlinzi wa Leicester City na Uingereza, Harry Maguire ameieleza klabu hio nia yake ya kuigura na kujiunga na Manchester United.

Maguire alikuwa na mazungumzo na kocha wake Brendan Rodgers pamoja na wachezaji wenzake wakiwa kwenye mazoezi ya kujiandaa kwa mechi za kirafiki kule Ufaransa.

Maguire anatarajia kuwa huenda jambo hilo litaharakisha mazungumzo baina ya klabu hizo mbili.

Kwenye dirisha la uhamisho lililopita, Maguire alishindwa kufanikisha uhamisho wake hadi Manchester United. Kwa sasa inatarajiwa kuwa Maguire atalazimisha uhamisho wake kwenda ugani Old Trafford.

Kando na Manchester United, Klabu ya Manchester City pia inawania sahihi ya mlinzi huyo. Hata hivyo, Manchester City huenda ikajiondoa kwenye harakati za kuwania sahihi yake kwani klabu ya Leicester inataka dau la millioni 75 ambalo ni sawia na walilotoa Liverpool ili kupata sahihi ya Virgil Van Dirk.

Maguire kwa sasa ni mmoja wa kikosi cha wachezaji 31 wa Leicester wanaojiandaa kwa mechi za kirafiki kwa ajili ya msimu mpya kula Ziwa Geneva nchini Ufaransa.

 Mwanzoni,Leicester City ilikataa kumuuza mlinzi wao mpaka wakati atasema kuwa anataka kuondoka yeye mwenyewe. Hatahivyo,Leicester City ilisema kuwa iwapo maguire atataka kuondoka basi hawatomzuia kufanya hivo.
https://radiojambo.co.ke/sababu-ya-vera-kubadilisha-rangi-yake/
Kikosi cha Leicester kinawalinzi wa kutosha na kulingana naye Brendan Rodgers pesa ya mauzo yake Harry itatumika kuimarisha nafasi nyingine klabuni hapo. Jonny Evans, Wes Morgan, Benkovic na Caglar Soyuncu wote wataweza kuziba pengo lake Harry hata ingawa huenda Leicester ikamnunua James Tarkowski kutoka Burnley ama Lewis Dunk kutoka Brighton.

Mashetani wekundu kwa sasa wamo nchini Australia huku wakitarajia kufanya sajili angalau nyingine mbili kuongeza kwake Aaron Wan Bissaka na Daniel James. Kocha wa Manchester United,Ole Gunnar Solskjaer anawatamani viungo wawili huku Bruno Fernades wa sporting Lisbon na Sean Longstaff wa Newcastle wakiwa kwenye orodha yake.

Kwa sasa Manchester United imo kwenye harakati za kukijenga kikosi kipya baada ya kushuhudia msukosuko wa matokeo ndani ya misimu miwili iliyopita.

soma pia:

View Comments