th

Kiungo Mshambulizi wa Manchester United Andreas Pereira amesema kuwa yupo tayari kumwibia simu Paul Pogba ili asizungumze na mtu yeyote kuhusu uhamisho wake kutoka Manchester United kwenda klabu nyingine yeyote ile.

'Huenda nikamwibia rununu yake ili aswiweze kuzungumza na mtu yeyote!'

Pereira akizungumza baada ya mechi baina ya kirafiki ya Manchester United na Leeds United.

Kwa muda sasa, Paul Pogba amekuwa akihusishwa na uhamisho kurejea nchini Italia kukipiga na Juventu pamoja na Uhamisho kuelekea Real Madrid ya Uhispania. Kulingana na ye Pereira, Pogba anauwezo wa kuwasaidia wachezaji wachanga kama yeye na Mason Greenwood.

"Pogba ni mtu mzuri sana.Litakuwa jambo la maana sana iwapo atakubali kubaki nasi hapa. Bila shaka Paul ni mcheza mwenye uwezo wa aina yake  nami nimeyajua mengi kutoka kwake. Tumekuwa naye tangia nikiwa na umri wa miaka 16 na ni rafiki wangu wa karibu kwa hivyo kwangu mie Pogba ni kama mmoja wa wanafamilia yangu,' Pereira alisema.

View Comments