- fs
- GFS
- HGFY
- D__vfN5XYAABpIs

Mkurugenzi mkuu wa shirikisho la FKF Robert Muthomi, amejiuzulu baada ya kuhusishwa na madai ya kuhusika na uhamisho wa mshambulizi wa Sofapaka John Avire kuelekea nchini Misri.

Muthomi ameipa nafasi shirikisho la FKF kuemdeleza uchunguzi dhidi ya madai hayo.

Brian Otieno, Katibu mkuu wa FKF amedhibitisha kuwa shirikisho la soka nchini limepokea malalamishi kutoka kwa mkuu wa Sofapaka Elly Kalekwa kumuhusu Robert Muthomi.

Hata hivyo, Muthomi amesema kuwa aliingilia madai yake Avire ilikusuluhisha matatizo ya mshahara baina ya klabu ya sofapaka na Avire ila sio kwa ajili ya kuendekleza shughuli zozote za uhamisho wa msham, bulizi huyo.

Avire aliyecheka na nyavu mara saba msimu uliopita amehusishwa na uhamisho kuelekea klabu moja ya ligi kuu nchini Misri ambayo haikutajwa.

Mkurungenzi mkuu wa FKF Robert Muthomi alisema kuwa kulikuwa na mazungumzo na klabu moja ya Misri iliyokuwa tayari kutoa kitita cha pesa ndefu ilikupata huduma zake Avire.

Baada ya kurejea nchini kutoka mecvhi za AFCON, Avire alirejea nchini Misri kuitazama mechi ya fainali huku pasipoti yake ikisema kuwa alitarajiwa kurejea nyumbani mnamo tarehe 26 jambo lililoimbua vurugu nyingi kwenye kambi ya Sofapaka. Kulingana naye kocha mkuu wa sofapaka, Echesa, Avire alitarajiwa kurejea mazoezi kama wachezaji wengine.

Awali kulikuwako na malalamishi kutoka kwa mshabiki wa Harambee Stars kuhusiana na Uamuzi wa kocha kumwacha Jesse Were pamoja na Allan Wanga kwa ajili ya John Avire kwenye mechi za AFCON.

View Comments