Meneja wa Chelsea Frank Lampard ametetea uteuzi wa kikosi chake kilichoshiriki mchuano wa Jumapili walionyukwa mabao 4-0 na Manchester United unwanjani Old Traford, wakati akijibu matamshi ya aliyekuwa meneja wa timu hiyo Jose Mourinho.

Mourinho alionekana kwa mara ya kwanza kama mchanganuzi wa mechi katika Sky Sport siku ambayo Lampard aliyekuwa wakati mmoja kiungo katika kikosi cha Mourinho aliongoza Chelsea katika wadhifa wa meneja katika mchuano wake wa kwanza wa ligi ya primia.

Mkufunzi huyo raia wa Ureno, aliyefutwa na Manchester United mwezi Disemba, alikuwa akiwakashifu wachezaji wa wanchester United Marcus Rashford na Anthony Martial kabla ya mchuano baina yao na Chelsea.

Rashford alifunga mabao mawili katika mchuano huo huku Martial akipachika wavuni lake moja, mchezaji mpya Dan James pia alifungua ukurasa wake wa mabao uwanjani Old Traford. Lakini Mourinho alihoji ikiwa wachezaji hao wataendelea kucheza vyema dhidi ya wapinzani wa hadhi ya juu.

“Nafikiri wanaweza wanapocheza dhidi ya timu kama vile Chelsea, nadhani walikuwa wanyonge,” Mourinho alisema, kabla ya kuhoji mfumo uliotumiwa na Lampard.

“(Chelsea) haikuwa thabiti katika safu ya ulinzi, nafasi kubwa mno kwa mpinzani kucheza, hawakuwa na msukumo kwa mpira, safu ya ulinzi, kiungo, mashambulizi, hawakuwa na mshikamano,” alisema.

“(mbele ) Tammy Abraham alikuwa akisalia mbele, (Ross) Barkley alikuwa akisalia mbele,  (Mason) Mount alikuwa akisalia mbele , Pedro alikuwa akisalia mbele.

Frank Lampard ateuliwa meneja mpya wa Chelsea

Mourinho alihoji uteuzi wa kikosi na Lampard, hasa uamuzi wake kumchezesha N'Golo Kante, aliyekuwa anarejea baada ya kupona tu jeraha.

Lampard alionekana kushangazwa na matamshi ya Mourinho, hasa kuhusiana na uamuzi kumchezesha Mount mwenye umri wa miaka 20 aliyekuwa anacheza mechi yake ya kwanza ya ligi ya primia.

TAARIFA IMETAFSIRIWA NA DAVIS OJIAMBO

View Comments