messi and ronaldo

Kwa kawaida droo za mechi na hafla za tuzo huenda zikajivuta kwa hotuba ndefu na kukosa msisimko.

Lakini zinapo wakutanisha wachezaji wawili bora duniani - Lionel Messi na Cristiano Ronaldo - ambao wamekubaliana kukaa chini pamoja na kupata mlo wa jioni, hugeuka kuwa kitu kingine tofauti.

Kulikuwa na ucheshi baina ya kiungo wa mbele wa Juventus Ronaldo na mwenziwe wa Barcelona Messi walipotaniana na kuchekeshana wakiwa wamekaa karibu pamoja.

Ilikuwa vigumu hata kuwafikiria wawili hao kwamba waliwahi kuwa mahasimu wakuu katika kipindi cha miaka 9 ya Ronaldo akiwa Real Madrid katika muongo mmoja uliopita wa kura ya kuwania tuzo ya Ballon d'Or ya mchezaji bora duniani wa soka.

"Tumekuwa katika jukwaa hili pamoja kwa miaka 15 years. Sijui kama hilo limewahi kufanyika katika siku za nyuma - watu hao hao wawili katika jukwaa hili wakati wote," Ronaldo amesema.

"Bila shaka tuna urafiki mzuri. Hatujawahi kula meza moja, lakini natarajia hilo litafanyika katika siku zijazo.

"Tulikuwa na ushindani huo Uhispania. Nilimshinikiza na yeye akanishinikiza mimi pia. Kwahivyo ni vizuri kuwa sehemu ya historia ya soka."

Kwa mapenzi kama haya , nani anayeweza kuthubutu kusema kwamba kuna uhasama kati ya wawili hawa?

Enzi za Cristiano Ronaldo na Lionel Messi za kutawala tuzo za mpira zinaendelea kusukumwa ukingoni, na usiku huu beki wa Liverpool na Uholanzi Virgil van Dijk amewaangusha.

Van Dijk amenyakua tuzo ya mchezaji bora wa bara Ulaya kwa mwaka 2018/19 Van Dijk baada ya kuingoza safu ya ulinzi ya Liverpool kuchukua Champions League msimu uliopita.

Van Dijk amekuwa baraka kwa Liverpool tangu alipojiunga na klabu hiyo kutoka Southampton na amekuwa kiungo muhimu kuisaidia kushinda Champions League msimu uliopita na pia kuisaidia kuwania taji la Ligi ya Premia dhidi ya Manchester City hadi mwisho.

-BBC

View Comments