sanchez

Alexis Sanchez anasema alishawishiwa kujiunga na Inter Milan na aliyekuwa mchezaji mwenzake wa Manchester United Romelu Lukaku. Sanchez alijiunga na Inter kwa mkopo wiki kadha baada ya Lukaku kukamilisha uhamisho wake wa kudumu kwenye klabu hio.

Sanchez anatumai kufufua tajriba yake Italia, ambapo awali alichezea Udinese kwa ufanisi. Anasema aliyekua meneja wa Chelsea Antonio Conte na Lukaku walimshawishi kuregea Serie A. Sanchez alikubali kujiunga na Inter baada ya kukosana na meneja wa United Ole Gunnar Solskjaer.

Eden Hazard na nduguye Thorgan watakosa michuano ya Ubelhiji ya kufuzu kwa Uro mwaka 2020 dhidi ya Scotland na San Marino kutokana na majeraha. Timu hio ya Roberto Martinez ambayo tayari imekumbwa na kujiondoa kwa baadhi ya wachezaji watacheza San Marino alhamisi kabla ya kutembelea Hampden Park Jumatatu.

Jeraha la msuli limemzuia Eden Hazard kuchezea Real Madrid tangu ahamie huko kutoka Chelsea. Thorgan naye alipata jeraha la mbavu akichezea Borussia Dortmund.

Mlinzi wa Manchester City Aymeric Laporte amefanyiwa upasuajai wa goti, uliofaulu baada ya kuondolewa uwanjani kwa machela wakati wa mechi yao waliyoshinda 4-0 dhidi ya Brighton Jumamosi.

Mfaransa huyo alianguka alipogongana na kiuongo wa Brighton Adam Webster kunako dakika ya 34 ya mechi hio ugani Etihad Stadium. Laporte alichaguliwa hivi majuzi kwa kikosi cha Didier Deschamps' cha Ufaransa kwa michuano ijayo ya kufuzu kwa Uropa dhidi ya Albania na Andorra.

View Comments