- dzeko (1)
- green (1)
- wilcok (1)
- europa-1

Ligi ya Europa ambayo iling'oa nanga jana ulishuhudia ushindani mkubwa huku klabu tofauti zikishamiri, zingine zikiadhibiwa.

EINTRACHT VS ARSENAL

Vijana wake Unai Emery waliwaadhibu wachezaji wa Eintracht nyumbani kwao mabao tatu kwa bila.

Willcock mshambulizi mwenye umri mdogo wa arsenali alitikisa nyavu dakika ya 38, huku Saka na Aubemeyang wakiongeza mabao katika dakika ya 85, na 87 mtawalia.

Mchezaji wa Eintracht Kohr alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 79, baada ya kucheza visivyo.

MANCHESTER UNITED VS ASTANA

Man united waliwakaribisha Astana nyumbani kwao Oldtrafford na kuwaadhibu bao moja kwa bila ambayo ilifungwa na mchezaji Greenwood dakika ya 73, dakika za lala salama.

United walitawala sana katika mchuano huo kwani walijaribu mara 20 kutafuta bao huku wapinzani wao Astana wakikosa kupata nafasi hata moja ya kufunga  vijana hao wa Ole Gunnar Solsjaer.

ROMA VS ISTANBUL BASAKSEHIR

Ni mechi iliyoshuhudia klabu ya Roma ikitikisa nyavu mara nne kupitia wachezaji Dzeko, Zaniolo, na Kluivert katika dakika ya 58, 71, na 90 mtawalia huku mchezaji wa Istanbul Junior Caicara akijifunga bao katika dakika ya 42.