- elazalkmaarmanutd031019
- elazarsenalstandardliege031019
- eufa europa

Raundi ya pili ya ligi ya Europa itakuwa inachezwa leo usiku huku klabu mbali mbali kutoka bara hilo wakitarajia kughubia pointi tatu.

Vijana wake Ole Gunnar Solsjaer watakuwa wanasafiri hadi uwanjani Afas Stadion nyumbani kwake klabu ya AZ Alkmaar.

Man United ambao walitoka sare tasa na klabu ya Arsenal katika ligi ya Uingereza wiki hii, wanatarajiwa kushamiri katika mechi hiyo ili waweze kuongoza katika kundi hilo, kwani kwa sasa wanashikilia nafasi ya pili na pointi 3 nyuma yake klabu ya Partizan.

 Utabiri wangu ni mwana manchester atamnyuka AZ Alkmaar mabao matatu kwa moja.

Vile vile klabu ya Arsenal watakuwa wanachuana na Standard Liege klabu ambayo inacheza katika ligi ya Ubelgiji.

Unai Emery ambaye ni mkufunzi wa klabu ya Arsenali ana matumaini kuwa vijana wake watashinda mechi hiyo.

Kwa sasa klabu hizo mbili zinaongoza katika kundi lao huku wote wakighubia pointi tatu.

Je, nani ataibuka mshindi usiku wa leo?

 Utabiri wangu ni Arsenal watashinda mechi hiyo itakayochezewa uwanjani Fly Emirates kwa kufunga mabao 4-2.
View Comments