Coronavirus :Mchuano wa Barcelona v Napoli kuchezwa bila mashabiki
Mchuano wa kombe la mabingwa kati ya barcelona na Napoli tarehe 18 mwezi huu utasakatwa katika uwanja uliofungwa waa Nou Camp kwa ajili ya hofu ya virusi vya Corona .
" Uamuzi huo umefanywa kwa minajali ya sababu za kiafya’ amesema afisa mkuu wa afya wa serikali ya jimbo la Catalunya Joan Guix. Mchuano huo ni wa pili kati ya timu za uhuspania na italia katika ligi ya mabingwa kusakatwa bila mashabiki baada ya mchuano wa Valencia dhidi ya Atalanta jumanne wiki iliyopita . Mchuano wa Getafe na Inter Milan katika kombe la bara Uropa pia uliishia hatma hiyo .
Mchuano wa kombe la mabingwa kati ya Paris St-Germain na Borussia Dortmund siku ya jumatano pia utakosa mashabiki . shughuli zote za michezo nchini Italia zimesitishwa hadi Aprili tarehe 3 kwa ajili ya hofu ya virusi vya Corona . Agizo hilo litaathiri pia mechi za kombe la Serie A lakini sio timu za italia au vilabu vinavyoshiriki mashindano ya kimataifa.
Ripoti zaarifu kwamba La liga huenda ikatoa tangazo kwamba mechi zake zijazo zitasakatwa katika viwanja visivyokuwa na mashabiki . mchuano wa Manchester united wa kombe la bara uropa raundi ya 16 bora dhidi ya LASK Linz nchini Austria siku ya alhamisi huenda pia ukachezwa katika uwanja mtupu bila mashabiki