EWSSK5aWsAABe1J

NA NICKSON TOSI

Usimamizi wa klabu ya Derby inayoshiriki ligi ya divisheni ya pili Uingereza umethibitisha kuwa wafanyakazi wa klabu hiyo wakiwemo wachezaji wamekubali kupunguzwa mishahara ili kusaidia timu hiyo wakati huu ambapo hakuna shughuli zote za kandanda zinazoendelea.

Viongozi hao wamewasifia wachezaji Wayne Rooney na Curtis Davies kuhusiana na hatua yao kuzungumza na wachezaji wenza ili kuafikia uamuzi huo.

Mkurugenzi mkuu wa klabu hiyo Stephen Pearce amethibitisha hayo akisema kuwa hatua hiyo itasaidia pakubwa kwa klabu hiyo kuendelea na shughuli zake za kawaida baada ya msimu kusitishwa.

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO

View Comments