images

Bruno Fernandez alifungia Manchester United goli la ushindi katika dakika za lala salama kupitia mkwaju wa penati na kuilaza Brighton 3-2 katika ligi ya  EPL.

Kwingineko, Tammy Abraham alitia kimyani goli la kusawazisha katika dakika ya 93 na kisaidia Chelsea kutoka sare ya 3-3 na West Brom baada ya wapinzani wao kuongoza 3-0 katika kipindi cha kwanza.

Everton nao waliwabwaga Crystal Palace 2-1 na kusalia kileleni na alama 9 baada ya mechi tatu.

Lewis Hamilton alishinda mbio za majaribio ya mwisho katika msururu wa langa langa nchini Urusi baada ya kuwashinda Max Verstappen wa red bull na dereva mwenza wa Mercedes Valtteri Botas.

Bingwa huyo wa Dunia ambaye anawania kufikisha rekodi ya Michael Schumacher ya kushinda mbio sita za Dunia anatarajia ushindi Leo mjini Sochi, huku mashabiki 30,000 waki ruhusiwa kutazama moja kwa moja licha ya janga la Corona.

View Comments