In Summary

Atakumbukwa kwa kuchezea Madrid kwenye michuano 671 na kuisaidia kushinda ligi ya mabingwa barani Ulaya (Champions League) mara 4, LA LIGA 5,  Copa del Rey 2, kombe la Supercopa 4  na  UEFA Super Cup 3. 

Sergio Ramos
Image: Hisani

Hatimaye mlinzi  matata wa klabu ya Real Madrid atakuwa anaondoka baada ya kuichezea kwa  miaka 16.

Real Madrid ilitangaza kuwa hafla ya kumpa heshima na kumuaga ilifanyika mida ya saa sita unusu mchana (masaa ya Uingereza) siku ya Jumatano.

Hata hivyo, haikuwekwa wazi Mhispania huyo atakuwa anajiunga na klabu ipi baada ya kuondoka.

Mchezaji huyo wa miaka35 alijiunga na mabingwa mara 34 wa Laliga, Real Madrid, mwaka wa 2005 kutoka klabu ya Sevilla.

Ndani ya kipindi cha miaka 16 ambayo amekuwa Madrid, Ramos ameshinda mataji si haba. Amelinganishwa na simba kutokana na ujasiri wake katika safu ya ulinzi na kote uwanjani.

Ramos ameweka rekodi ya mabao mengi sana na klabu hiyo, mabao 101,  jambo ambalo si la kawaida kwa walinzi.

Atakumbukwa kwa kuchezea Madrid kwenye michuano 671 na kuisaidia kushinda ligi ya mabingwa barani Ulaya (Champions League) mara nne, kombe la LA LIGA kwa mara tano, mataji mawili ya Copa del Rey, kombe la Supercopa mara nne na taji la UEFA Super Cup kwa mara tatu.

Amekuwa  nahodha wa klabu hiyo tangu mwaka wa 2015 baada ya kuondoka kwa mlinda lango, Iker Casillas.

Ramos anakisiwa kurudi tena kwa klabu yake asili Sevilla ama kujiunga na PSG ya Ufaransa au Manchester United ya Uingereza.

View Comments