In Summary

•Klabu ya Gor Mahia imetoa wito kwa mashabiki na wasamaria wema kutoa mchango ili kusuluhisha matatizo ya fedha.

•Klabu hiyo imepeana nambari ya kulipia huduma 4025683 na nambari ya akaunti Gor Mahia F.C.

divas

Klabu ya Gor Mahia imetoa wito kwa mashabiki na wasamaria wema kutoa mchango ili kusuluhisha matatizo ya fedha.

Kupitia ujumbe uliotolewa kwa wanahabari asubuhi ya Jumatatu, klabu hiyo imewahimiza wanachama wa klabu, mashabiki na wasamaria wema kutoa michango ya kila mwezi ya kiwango cha pesa ambacho wataweza.

Kulingana na ujumbe huo ambao umetiwa saini na mwenyekiti wa Gor Mahia, Ambrose Rachier, maafikiano hayo yamejiri kufuatia matatizo ya fedha ambayo yamesababishwa na janga la Korona.

"Kamati ya utendaji imeangazia mifumo mbalimbali inayotumika na klabu ambazo zimefanikiwa kote ulimwenguni na kuamua kutumia baadhi yake ili kuanzilisha  mpango wa kuchanga pesa utakaohakikisha uendelevu wa klabu kwenye siku za usoni" Rachier alisema.

Rachier alisema kuwa mpango huo utasaidia kusuluhiha matatizo ya fedha ambayo yamekuwepo hapo awali.

Klabu hiyo imepeana nambari ya kulipia huduma 4025683 na nambari ya akaunti Gor Mahia F.C.

Rachier alisema kuwa wataendelea kufanya mipango ya kuletea klabu hiyo pesa kupitia kushirikiana na wanachana katika uwekezaji.

View Comments