In Summary
  • Shirikisho la soka Tanzania lampiga marufuku mwanahabari maarufu
Image: TFF

Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF limempiga marufuku mwanahabari maarufu nchini humo kwa kipindi cha miaka mitano kwa kuchapisha habari za uwongo pamoja na zile za uchochezi.

Shirikisho hilo linasema kwamba Shaffih Dauda hawezi kushirikishwa katika masuala yoyote ya soka ndani au nje ya taifa hilo.

Pia amepigwa faini ya $2,500. Bwana Dauda hajatoa matamshi yoyote rasmi. Taarifa iliochapishwa katika mtandao wake wa Instagram wiki iliopita imeondolewa.

Mbali na kuwa mwanahabari, Bwana Dauda pia ni mwanachama wa kamati kuu ya TFF.

Pia anafanya kazi kama skauti wa soka na alikuwa na jukumu kubwa katika uhamisho wa Mbwana Samatta kutoka KRC Genk ya Ubelgiji hadi Aston Villa mwaka 2020 na kumfanya kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza ligi kuu ya Uingereza.

View Comments