In Summary

•Huku akipokea $130 million kabla ya kutozwa kodi , katika kipindi cha miezi 12 iliopita, Messi anashikilia nafasi ya kwanza katika orodha ya jatrida la Forbes.

Messi apokea tuzo la mchezaji bora kwa mara ya 7
Image: BALLON D'OR TWITTER

Lionel Messi anaongoza kundi la watu ambalo kwa pamoja wamekuwa wakijipatia zaidi ya $990m katika miezi 12 , huku kiwango cha kuwania nafasi hiyo kikipanda zaidi ya ilivyokuwa awali.

Lionel Messi alikuwa na umri wa miaka 17 alipoanza kushiriki katika kikosi cha kwanza cha timu ya Barcelona , hivyobasi aliondoka katika klabu hiyo baada ya miaka 17 na kujiunga na klabu ya PSG Agosti iliopita.

Huku akipokea $130 million kabla ya kutozwa kodi , katika kipindi cha miezi 12 iliopita, Messi anashikilia nafasi ya kwanza katika orodha ya jatrida la Forbes ya kila mwaka dunianoi akiwa mchezaji anayelipwa zaidi akiongozo orodha hiyo kwa mara ya pili baada yam waka 2019.

Ingawa Forbes wanakadiria kuwa mshahara wa Messi umepungua takriban dola milioni 22 kutoka mwaka wake wa mwisho akiwa na Barcelona hadi dola milioni 75 msimu huu akiwa PSG - nyongeza kubwa ya uidhinishaji inamsaidia kufikia rekodi ya jumla ya miezi 12 ya mchezaji wa soka aliyochapisha mwaka jana, wakati alipomaliza katika nafasi ya 2 nyuma ya mpiganaji wa MMA Conor McGregor.

Mpinzani wa Messi, Cristiano Ronaldo-ambaye pia alibadilisha timu mwezi Agosti, akihama kutoka Juventus kwenda Manchester United-ameorodheshwa wa tatu mwaka huu akiwa na $115 milioni. Aliye katikati ya wawili hao ni mchezaji wa timu ya vikapu ya La lakers LeBron James aliyepokea $121.2 milioni, na kuvunja rekodi ya $96.5 milioni ya mchezaji wa NBA ambayo aliweka mwaka jana. James anakuwa mwanariadha wa kumi pekee kuwahi kupita dola milioni 100 kwa mwaka mmoja, hatua ambayo Messi na Ronaldo wamefikia mara tano kila mmoja.

Wachezaji wanaopokea fedha nyingi zaidi duniani 2022.

#1 | $130 MILLION

LIONEL MESSI

Image: GETTY IMAGES

Umri: 34 | mchezo: kandanda | Uraia: Argentina

Ushirikiano wa Lionel Messi wa $20 milioni kwa mwaka na Socios unaongeza kwenye jalada la mapato linalojumuisha Adidas, Budweiser na PepsiCo. Pia alikuwa balozi wa kwanza wa kampuni ya Hard Rock International katika mkataba uliotangazwa Juni mwaka jana, hali iliomsaidia kuwa sawa na Cristiano Ronaldo wa Manchester United kutokana na mapato yake ya nje ya uwanja kwa mara ya kwanza tangu 2013. Messi alishinda taji la Ballon d'Or mwaka 2021 kama mchezaji bora soka upande wa wanaume duniani, lakini amekuwa na wakati mgumu zaidi uwanjani hivi majuzi, akifunga mabao tisa pekee katika mechi 32 akiwa na Paris Saint-Germain baada ya kufikisha mabao 38 katika michezo 47 katika msimu wake wa mwisho akiwa Barcelona. Lakini wakati PSG wakipambana katika hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, klabu hiyo ilitwaa taji la Ligue 1 ya Ufaransa katika msimu wa kwanza wa Messi.

#2 | $121.2 MILLION

LEBRON JAMES

Lebron James
Image: BBC

Umri: 37 | Mchezo: Mpira wa vikapu | Uraia: Marekani

LeBron James' Los Angeles Lakers walikosa kushiriki katika mechi za mchujo msimu huu playoffs, lakini hajawahi kutawala sana nje ya uwanja. Aliigiza katika Space Jam: Hivi majuzi alihamisha kipindi chake cha mazungumzo, The Shop, kutoka HBO hadi mtandao wa YouTube. Mnamo Oktoba, aliuza hisa nyingi katika SpringHill-kampuni ya uzalishaji ilioanzisha miradi yote miwili-kwa thamani ya takriban $725 milioni, na kusukuma thamani yake kufikia $850 milioni, kulingana na makadirio ya Forbes. Baada ya kutangaza mpango wa makubaliano na Crypto.com mnamo Januari, James alionekana kwenye tangazo la Super Bowl karibu na toleo la kompyuta la mdogo wake. Pia hivi majuzi aliwekeza katika kampuni ya mazoezi ya nyumbani ya Tonal na StatusPRO, uanzishaji wa teknolojia ya michezo ambao huunda bidhaa za kufanyia mazoezi.

#3 | $115 MILLION

CRISTIANO RONALDO

Manchester United imebanduliwa kutoka Champions League
Image: GETTY IMAGES

MANCHESTER UNITED FC

Umri: 37 | Mchezo: kandanda | Uraia: Portugal

Sawa na mpinzani wake Lionel Messi, Cristiano Ronaldo amekuwa na msimu wa kwanza wa kusikitisha akiwa na timu yake mpya Manchester United katika nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza ikiwa imesalia na mchezo mmoja. Uvumi sasa unaenea kwamba Ronaldo, ambaye aliichezea Man U hapo awali kutoka 2003 hadi 2009, anaweza kuhama kwa mara nyingine katika dirisha hili la usajili . Mapato mengi ya Ronaldo yanatokana na uwepo wake mkubwa kwenye mitandao ya kijamii: Ana wafuasi milioni 690 kwenye Instagram, Facebook na Twitter, na hivyo kumpa nguvu ya kudai mapato ya viwango vya juu kutoka kwa wafadhili kama vile Nike, Herbalife na Clear shampoo. Yeye pia ni mwekezaji katika mikahawa ya Tatel—pamoja na eneo jipya huko Beverly Hills—na ndiye uso wa ZujuGP, programu inayolenga kuwa kituo kikuu cha kijamii cha soka ya kidijitali.

#4 | $95 MILLION

NEYMAR

Neymar Junior
Image: BBC

Umri: 30 | Mchezo: kandanda | Uraia: Brazil

Neymar alifunga bao lake la 400 katika maisha yake ya soka mwezi Novemba, lakini kama Lionel Messi, alikasirishwa na shutuma baada ya Paris Saint-Germain kuondolewa mapema katika Ligi ya Mabingwa. Mawazo yake sasa yatahamia Kombe la Dunia huko Qatar mwisho wa msimu huu ambao amesema unaweza kuwa wa mwisho kwake. Nje ya uwanja, ana ufadhili muhimu, unaojumuisha kampuni za Puma na Red Bull, na ndiye mhusika wa toleo jipya la Netflix, Neymar: The Perfect Chaos. Pia ameingia katika ulimwengu wa NFTs, akiafikia makubaliano na jukwaa la NFTSTAR mnamo Novemba na kutumia zaidi ya $1 milioni kununua mabot ya kifahari kwa siku moja mnamo Januari

#5 | $92.8 MILLION

STEPHEN CURRY

Stephen Curry
Image: BBC

Umri: 34 | Mchezo: Mpira wa vikapu | Uraia: Marekani.

Hakuna mchezaji wa NBA aliyelipwa zaidi msimu huu kuliko Stephen Curry, na mchezaji huyo wa timu ya Golden State Warriors anatazamiwa kuongezwa mapato yake baada ya kusaini nyongeza ya miaka minne ya thamani ya $215 milioni Agosti mwaka jana. Atajipatia takriban dola milioni 48 uwanjani msimu ujao, na kupanda hadi chini ya dola milioni 60 mnamo 2025-26. Mkataba mpya wa ufadhili wa FTX wa Curry pia ulikuja na dau la hisa, na aliingia zaidi kwenye blockchain mnamo mwezi Desemba, akitoa mkusanyiko wa NFTs ambao ulioshirikisha viatu vyake vilivyofungwa kwenye majukwaa matatu ya metaverse. (Aliahidi kutoa kama mchango mapato hayo.) Wakati huo huo, kampuni ya ya Curry, Unanimous Media, ilitia saini mkataba wa maendeleo na Comcast NBCUniversal mwezi Septemba.

#6 | $92.1 MILLION

KEVIN DURANT

kelvin Durant
Image: BBC

Umri: 33 |Mchezo: Mpira wa vikapu| Uraia: Marekani

Nyota wa timu ya vikapu ya Brooklyn Nets Kevin Durant hujipatia takriban dola milioni 28 kila mwaka kutoka kwa Nike, mikataba ya sneakers ambayo inazidiwa tu na ile ya LeBron James' yenye thamani ya ($ 32 milioni) kati ya wachezaji wanaocheza. Hivi majuzi ameongeza mikataba na Coinbase, NBA Top Shot na Weedmaps, lakini akiwa na kampuni ya habari ya Boardroom na kampuni ya uwekezaji ya Thirty Five Ventures, ufalme wake wa biashara umepanuka zaidi ya ilivyokuwa. Durant na mshirika wake wa muda mrefu wa biashara, Rich Kleiman, pia walitangaza mwaka jana kwamba wangezindua SPAC yao wenyewe.

#7 | $90.7 MILLION

ROGER FEDERER

Roger Federer
Image: BBC

Umri: 40 | mchezo: Tennisi | Uraia: Switzerland

Injuries limited Roger Federer to six tournaments in 2020 and 2021 combined, and he has yet to return to the tennis court in 2022. No matter—the world's former No. 1 player remains the top pitchman in sports, promoting brands such as Uniqlo and Rolex. He also invested in the burgeoning Swiss shoe brand On in 2019, and the company went public in September, raising more than $600 million. "We work very closely together on product design," Federer told Forbes at the time, having spent 20 days in the lab with the On team developing the company's pro tennis shoe.

#8 | $90 MILLION

CANELO ALVAREZ

CANELO ALVAREZ
Image: BBC

Umri: 31 | Mchezo: Ndondi | Uraia: Mexico

Canelo Alvarez ndiye bondia bora wa ndondi, akipata dola milioni 40 au zaidi kutokana na ushindi wake wa mara mbili mwezi Mei na Novemba. (Kupoteza kwake dhidi ya bingwa wa uzani wa light-heavyweight Dmitry Bivol mnamo Mei 7, 2022, kulitokea nje ya dirisha la Forbes la orodha hii.) Zaidi ya ulingo, Alvarez ana ushirikiano mzuri na Hennessy na anamiliki mkahawa wa taco katika nchi yake ya asili ya Mexico, akiwa na mipango kuwekeza hadi California. Alvarez alisema mwaka jana kuwa atakuwa akizindua msururu wa vituo vya mafuta, na kampuni yake ya Canelo Promotions inaandaa msururu wa mapambano nchini Mexico kwa ushirikiano na Matchroom Boxing na DAZN.

#9 | $83.9 MILLION

TOM BRADY

Tom Brady
Image: BBC

Umri: 44 | Mchezo: soka ya Marekani | Uraia: Marekani

Kustaafu kwa Tom Brady katika msimu huu kulidumu kwa chini ya wiki sita, ambazo zilikuwa habari njema kwa timu Tampa Bay Buccaneers baada ya kusajiliwa katika msimu wa 2021 akiwa na umri wa miaka 43. Hakika anajifunza mbinu mpya nje ya uwanja. Brady tayari ana tamasha lake la faida kubwa lililopangwa: jukumu la kutoa maoni na Fox Sports. Kulingana na New York Post, dili hilo linatazamiwa kumlipa zaidi ya alizopata uwanjani katika misimu 22 ya NFL—dola milioni 375 kwa miaka kumi.

#10 | $80.9 MILLION

GIANNIS ANTETOKOUNMPO

Giannis Antetokounmpo
Image: BBC

Umri: 27 | Mchezo: Mpira wa vikapu | Uraia: Ugiriki

Huku Neymar akifikisha miaka 30 mwezi Februari, Giannis Antetokounmpo ndiye mshiriki pekee wa kumi bora mwaka huu ambaye bado yuko umri wa miaka 20. Kijana huyo aliyejishindia taji la mchezaji bora yani MVP mara mbili akiichezea Milwaukee Bucks alitia saini mkataba wa miaka mitano wa $228 milioni mnamo Desemba 2020, mkataba mkubwa zaidi wa NBA kwa thamani ya jumla hadi sasa. Alikuwa miongoni mwa wawekezaji katika awamu ya ufadhili ya WatchBox ya kuuza saa milioni 165 iliyotangazwa mnamo Novemba, na pia amesaini mkataba wa leseni na jukwaa la NFT NFTSTAR na kuongeza WhatsApp na simu ya Google ya Pixel 6 kwenye kmapuni zinazomfadhili. Na Antetokounmpo hivi karibuni ataweza kutazama hadithi yake ya maisha katika Rise ya kibayolo

  

View Comments