logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanariadha Agnes Jeruto apigwa marufuku ya miaka 5 kwa kutumia dawa za kusisimua misuli

Agnes, mwenye umri wa miaka 41 ni mwanariadha wa mbio za masafa marefu.

image
na Davis Ojiambo

Michezo11 September 2023 - 12:28

Muhtasari


  • • AIU imemuzuia mwanariadha Agnes Jeruto kushiriki katika mbio kwa miaka mitano kwa kosa la kutumia dawa za kusisimua misuli.
  • •Mwanariadha huyo  alishinda toleo la kwanza la Nairobi City Marathon mwaka wa 2022 na pia ni mshindi wa Hangzhou Marathon mwaka wa 2019.
Agnes Jeruto/Facebook

Kitengo cha Uadilifu cha Riadha AIU kimemuzuia mwanariadha Agnes Jeruto kushiriki katika mbio kwa miaka mitano kwa kosa la kutumia dawa za kusisimua misuli.

Agnes, mwenye umri wa miaka 41 ni mwanariadha wa mbio za masafa marefu.

Katika taarifa AIU ilibaini kuwa Jeruto alitumia dawa iliyopigwa marufuku ya kuongeza damu baada ya vipimo vya maabara.

Japo kosa hilo linafaa kutumikia miaka minne, Agnes atatumikia mwaka mmoja zaidi kutokana na uzito wa ukiukaji huo. Marufuku hayo yalianza septemba 6, mwaka huu ambapo uamuzi ulitolewa.

AIU, ilibaini kuwa matokeo yaliyounganishwa na pasipoti ya mwanariadha huyo yalionyesha ushahidi wa matumizi ya dawa ambazo zimepigwa marufuku kwa wanariadha zenye wakala wa uchangamshi kama vile recombinant erythropoietin, au mbinu yeyote iliyopigwa marufuku mara nyingi.

Taarifa ya AIU ilisoma;

"Kuongezeka kwa muda unaotumika vinginevyo wa kutostahiki kwa miaka minne (4), kwa muda wa ziada wa miaka miwili (2) kulingana na uzito wa ukuikaji na asili ya hali mbaya,"

Kulingana na AIU, mwanariadha huyo alikiri ukiukaji wa sheria ya kupinga matumizi ya dawa za kusisimua misuli na hivyo kupunguziwa muda wa mwaka mmoja katika kipindi chake cha marufuku.

Kwa hivyo kulingana na sheria za AIU;

"Mwanariadha atapokea punguzo la mwaka mmoja (1) katika kipindi kinachodaiwa cha kutostahiki kwa mujibu wa kanuni ya 10.8.1 iwapo atakiri mapema na kukubaliana kwa adhabu,"

Mwanariadha huyo  alishinda toleo la kwanza la Nairobi City Marathon mwaka wa 2022 na pia ni mshindi wa Hangzhou Marathon mwaka wa 2019.

AIU imearifu kuwa sampuli za damu zilichukuliwa kutoka kwa wanariadha kumi na wawili (12) kati ya tarehe 10 julai 2013 na Novemba 30, 2022, na kupelekwa kwa mahabara  na kupata majibu hayo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved