Bondia wa Nigeria Cynthia Ogunsemilore ameondolewa katika Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024 baada ya vipimo kuonyesha kuwa ametumia dawa ya kusisimua misili.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 ni mwanariadha wa pili kufeli mtihani wa dawa kwenye Michezo ya Paris.
Ogunsemilore alitarajiwa kucheza mechi yake ya kwanza ya Olimpiki siku ya Jumatatu katika kitengo cha kilo 60 cha wanawake lakini sasa ndoto yake imesitishwa kufuatia ukiukaji wa kupinga matumizi ya dawa za kusisimua misuli.
Shirika la kimataifa la kukabiliana na utumizi wa dawa michezoni linasema sampuli ya nje ya shindano ilikusanywa tarehe 25 Julai na siku mbili baadaye ripoti ilionyesha matokeo chanya kwa furosemide iliyopigwa marufuku ambayo inaainishwa kama dawa ya kusisimua misuli.
Mnigeria huyo alishinda dhahabu katika Michezo ya Afrika mjini Accra mwaka huu na pia ni mshindi wa medali ya Jumuiya ya Madola.
Bondia huyo anaweza kukata rufaa dhidi ya matokeo lakini uamuzi wowote hautakuja kwa wakati kwa ili kumwezesha kushiriki mashindano ya sasa.
Matokeo ya Ogunsemilor yanamaanisha kuwa Nigeria sasa imesimamisha wanariadha kwa ukiukaji wa matumizi ya dawa za kusisimua misuli katika michezo miwili ya Olimpiki kufuatia mwanariadha Blessing Okagbare kufanyiwa majaribio miaka mitatu iliyopita mjini Tokyo.