In Summary
  • “Nilipokuwa Ikulu, nilimuahidi rais na nchi nzima kwamba ningemnunulia babangu gari jipya kutokana na mapato ya tuzo ya urais.
  • Baba wa mwanariadha kwa upande wake alibaini kuwa sasa anamiliki gari lake la kwanza, kwa hisani ya mafanikio ya binti yake.
Image: KWA HISANI

Mwanariadha aliyevunja rekodi ya dunia  ya mita 1500 na 5000 Faith Kipyegon hatimaye ametimiza ndoto yake ya babake kumiliki gari.

Ndoto hiyo ilitimia Jumamosi, Juni 17 wakati kampuni ya RANA Auto Motors, muuzaji magari yenye matawi yaliyoenea kote nchini ilipompa babake mwanariadha zawadi ya gari.

Sultan Rana, Mkurugenzi Mtendaji wa RANA Auto Motors alimkabidhi babake mwanariadha huyo mjini Eldoret.

Rana alibainisha kuwa alifanya uamuzi wa kutoa gari hilo na kutimiza ndoto ya Kipyegon "kama jukumu linalowekezwa kwa watu wa Kenya".

"Tuliona ni busara kusimama na Faith baada ya utendaji wake bora katika wiki mbili zilizopita. Ameacha alama isiyofutika kama mmoja wa wakimbiaji wakubwa nchini na tunajivunia kushirikiana naye." Aliongeza Mkurugenzi Mtendaji.

Kwa upande wake, mshika rekodi ya dunia ambaye alikuwa miongoni mwa waliohudhuria alionyesha furaha na shukrani zake.

“Nilipokuwa Ikulu, nilimuahidi rais na nchi nzima kwamba ningemnunulia babangu gari jipya kutokana na mapato ya tuzo ya urais.

Hata hivyo, Rana Auto Selection iliona ni vyema kumtuza baba yangu. Nina hisia na nina furaha kwamba baba yangu sasa ataendesha gari lake mwenyewe,” Kipyegon alisema.

Baba wa mwanariadha kwa upande wake alibaini kuwa sasa anamiliki gari lake la kwanza, kwa hisani ya mafanikio ya binti yake.

"Hili ni gari la kwanza maishani mwangu. Nashukuru, imekuja wakati mwafaka ukizingatia umri wangu. Ninajivunia mafanikio ya binti yangu."

View Comments