In Summary

• Kipyegon anasherehekewa kwa kuvunja na kuandikisha rekodi mbili mpya katika mbio za mita 5000 na mita 1500 wiki mbili zilizopita.

KICC yawaka kwa picha za Faith Kipyegon
Image: Facebook//Safaricom

Usiku wa Jumatatu jingo la KICC ambalo ndio nembo ya jiji la Nairobi lilipambwa kwa picha za mwanariadha Faith Kipyegon zenye rangi za kupendeza kama njia moja ya kumsherehekea na kumtambua kwa juhudi zake za kuandikisha rekodi mbili mpya kwenye riadha.

Kipyegon anasherehekewa kwa kuvunja na kuandikisha rekodi mbili mpya katika mbio za mita 5000 na mita 1500 wiki mbili zilizopita nchini Italia na Ufaransa mtawalia.

Katika ukurasa wa Facebook, kampuni ya Safaricom ambao walikuwa mstari wa mbele katika kusherehehekea Kipyegon kwa juhudi hizo, walipakia rundo la picha hizo nzuri zikionesha picha ya Kipyegon kwenye kuta za vioo za jingo hilo lenye orofa 29.

“Usiku wa leo, tuliungana na Wakenya kusherehekea Mwenye Rekodi ya Dunia, Faith Kipyegon kwa mafanikio yake ya ajabu ya kuweka rekodi 2 mpya za dunia katika wiki. Alionyesha ulimwengu jinsi inafanywa na hatukuweza kujivunia zaidi. Pitia KICC, katika CBD ya Nairobi usiku wa leo na uangalie onyesho hili la kushangaza tunaposherehekea bingwa wetu. #MalkiaRekodi Duniani,” Safaricom waliandika.

Kusherehekewa kwake kunakuja wiki moja tu baada ya rais Ruto kukutana naye katika ikulu ya Nairobi ambapo alimpa zawadi ya jumba la kifahari lenye thamani ya shilingi milioni 6 pamoja na kitita cha shilingi milioni 5 taslimu.

Kipyegon kwa machozi ya furaha alimshukuru rais kwa zawadi hiyo, akisema kuwa naye amefikia ndoto yake ya kuishi Nairobi na pia kuweza kumnunulia babake gari ambalo alikuwa amemuahidi kabla ya kuelekea Uropa kushiriki mbio hizo zilizofanyika ndani ya wiki moja.

Lakini sik uchache baadae pia, kulikuwa na taarifa kwamba kampuni moja ya kuuza magari ilichukua jukumu la kutimiza ndoto ya Kipyegon kwa babake kwa kuwasilisha gari kwa mzee huyo kwa niaba ya Kipyegon.

View Comments