In Summary

• Omanyala alishinda mbio za mita mia moja jijini Brussels Ubelgiji katika mashindano ya Diamond League kwa kuandikisha muda wa sekunde 10.07.

• Faith Kipyegon aongoza jedwali la mita 800 upande wa wanawake Omanyala akishikilia nafasi ya pili kwa wanariadha wenye kasi ulimwenguni.

OMANYALA

Mwanariadha mwenye kasi zaidi barani Afrika Ferdinand Omanyala ameorodheshwa katika nafasi ya pili ulimwenguni msimu huu kwenye jedwali la wanariadha wenye kasi zaidi duniani.

Omanyala alishinda mbio za mita mia moja jijini Brussels Ubelgiji katika mashindano ya Diamond League kwa kuandikisha muda wa sekunde 10.07.

Baada ya msimu wa msururu wa mbio mwaka 2024, Omanyala ametua katika nafasi ya pili kwa kuandikisha muda bora wa msimu kwa maana wa sekunde 9.79.

Mwanariadha wa Jamaica Kishane Thompson ndiye bingwa kwa kuandikisha muda bora wa msimu  kwa kuweka rekodi ya sekunde 9.77 

Omanyala ametoshana na bingwa na Olimpiki ya 2024 jijini Paris, Ufaransa Noah Lyles kwa sekude 9.79 ila Mkenya huyo alimshinda kwa kuandikisha WIND bora ya +1.5 wakati Lyles aliandikisha WIND ya +1.0.

Katika nafasi ya 4 ni Fred Kerly wa Marekani, akifuatiwa na Oblique Seville wa Jamaica, kisha Akani Sambine wa Afrika Kusini na saba bora ikifungwa na Lmont Marcell Jacobs wa Italia.

Katika mbio za mita 800, Emmanuel Wanyonyi anaongoza jedwali hilo kwa kuandikisha muda bora wa msimu kwa kuweka rekodi ya dakika 1.41.11 .

Wakenya wenzake katika riadhaa hizo za mita 800 ni Aaron Kemei katika nafasui ya 7 kwa kuweka rekodi ya dakika 1.42.08 akifuatiwa na Wyclife Kinyamala kwa dakika 1.42.08 japo wametoshana.

Mkenya Koitatol Kidali katika mbio hizo za mita 800, anashikilia nafasi ya 11 kwa muda wa dakika 1.42.66.

Kwa upande wa kina dada Faith Kipyegon anaongoza kwa muda bora wa msimu akiweka rekodi ya dakika 3.49.04 akifuatiwa na Gudaf Tsegay kutokea Ethiopia  kwa kuweka muda bora wa msimu wa dakika 3.50.30.

Kwenye mbio za mita mia 800 upande wa wanawake, Waingereza wanashikilia nafasi za kwanza tatu, Mkenya Mary Moraa akiridhika na nafasi ya nne kwa muda bora wa msimu wa dakika 1.56.56.

View Comments