In Summary
  • Lampard avunja kimya baada ya kufutwa kazi na chelsea huku akisema kwamba hakupewa muda wa kutosha
  • Kocha huyo alifutwa siku ya jumatatu,awali alikuwa kiungo wa kati katika kilabu hiyo na anaiacha Chelsea katika nafasi ya 9 kwenye jedwali la ligi ya premia
Frank Lampard

Baada ya Chelsea kumfuta kazi kocha Frank Lampard baada ya kuwa hatamuni kwa miezi 18, hatimaye amevunja kimya na kusema kwamba hakupewa muda wa kuinoa klabu hicho.

Lampard ,mwenye umri wa miaka 42 awali alikuwa kiungo wa kati katika kilabu hiyo na anaiacha Chelsea katika nafasi ya 9 kwenye jedwali la ligi ya premia baada ya kushindwa wiki jana na Leicester City na wameshinda mchuano mmoja pekee katika mechi tano za ligi . Mchuano wake wa mwisho ulikuwa siku ya jumapili katika kombe la FA raundi ya nne ambapo waliishinda Luton mabao matatu kwa moja .

Lampard aliteuliwa kocha wa The Blues kwa mkataba wa miaka mitatu alipochukua nafasi hiyo kutoka kwa Maurizio Sarri julai mwaka wa 2019

 

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram  Lampard alikuwa na haya ya kusema baada ya kufutwa kazi.

"Ninajivunia ufanisi wangu na nijavunia wachezaji wa shule ya soka ambao wamejiunga na timu ya kwanza na kusajili matokeo bora. Hao ndio tegemo la klabu. Nasikitika sijakuwa na muda wa kutosha msimu huu kupeleka klabu mbele na kuirejeshea hadhi,"alisema.

Pia alitakia klabu hicho mafanikio katika maisha yao.

Aliwaongoza kumaliza katika nafasi ya nne katika fainali ya kombe la FA katika kipindi chake cha kwanza usukani .

The blues hata hivyo imejipata pabaya katika ligi ya premier baada ya kushindwa katika mechi za nane zilizopita .

View Comments