In Summary

•Foden alifunga mabao 9 kwenye ligi kuu, mabao 3 kwenye ligi ya mabingwa bara Ulaya, mabao mawili kwenye kombe la FA na mengine wawili kwenye kombe la Carabao.

•Trent Arnold wa Liverpool aliweza kunyakua ushindi huo kwenye msimu jana wa 2019/20.

Phil Foden akionyesha tuzo lake
Image: Twitter

Kiungo wa klabu ya Manchester City, Phil Foden ameshinda tuzo la mchezaji mchanga bora msimu wa 2020/21.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 ametuzwa tuzo la mchezaji mchanga bora la PFA baada ya kufungia mabingwa wa ligi kuu Uingereza jumla ya mabao 16 kwenye kombe mbalimbali.

Foden alifunga mabao 9 kwenye ligi kuu, mabao 3 kwenye ligi ya mabingwa bara Ulaya, mabao mawili kwenye kombe la FA na mengine wawili kwenye kombe la Carabao.

Mchezaji huyo ambaye ameweza kuanzishwa katika mechi 17 za ligi kuu ameeleza imani yake kwa mkufunzi Pep Guardiola huku akieleza kuwa safari ya kupenya hadi kikosi cha kwanza haijakuwa rahisi.

"Nimekuwa nikitia bidii kila uchao na nimeamini mkufunzi. Nimetia bidii kwenye vipindi zote za mafunzo na kutumai kupata nafasi ya kucheza na kujaribu kucheza vizuri wakati nimepewa ile nafasi" Foden alieleza wanahabari wa Man City.

Foden aliweza kuwapiku wachezaji wachanga wengine mashuhuri kama Bukayo Saka(19) wa Arsenal, Mason Mount(22) wa Chelsea, Mason Greenwood(19) wa Mancheter United na Trent Alexandar Arnold(22) wa Liverpool.

Trent Arnold wa Liverpool aliweza kunyakua ushindi huo kwenye msimu jana wa 2019/20.

Foden amesherehekea ushindi huo na kusema kuwa huo ni wakati maalum sana maishani mwake licha ya kupokea upinzani mkubwa kutokana na wachezaji wengi wachanga waliokuwa na msimu mzuri pia.

View Comments