In Summary

• Arsenal wako tayari kusikikiza ofa kwa ajili ya nahodha wake Pierre-Emerick Aubameyang, 32.

• Hawatamzuia iwapo mshambuliaji huyo wa Gabon iwapo atataka kuondoka kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.

Nahodha wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang.
Image: GETTY IMAGES

Arsenal wako tayari kusikikiza ofa kwa ajili ya nahodha wake Pierre-Emerick Aubameyang, 32, na hawatamzuia iwapo mshambuliaji huyo wa Gabon iwapo atataka kuondoka kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili. (Telegraph - subscription required)

Washika bunduki hao pia wamedhamiria kumuunga mkono kocha wa timu hiyo aliyeko kwenye shinikizo kubwa Mikel Arteta kufuatia vipigo viwili ilivyovipata timu hiyo kwenye ligi kuu England. (Mirror)

Mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy hatapunguza thamani ya mshambuliaji wa England Harry Kane,28 na yuko tayari hata kukataa ofa kubwa ya kuvunja rekodi ya uhamisho Uingereza inayokaribia £150m kutoka Manchester City. (Telegraph- subscription required)

Image: GETTY IMAGES
Chelsea wanafikiria kumchukua kwa mkopo kiungo wa Atletico Madrid na Hispania Saul Niguez, 26, wakati huo huo "the blues" imewapa mikataba mipya walinzi wake Antonio Rudiger, 28, wa Ujeruman na Mdenmark Andreas Christensen, 25.

Kiungo wa England Declan Rice, 22 amepanga kukataa ofa yoyote ya kusaini mkataba mpya kutoka klabu yake ya West Ham kama mgomo baada ya klabu hiyo kumuwekea bei ya juu na kuweka ugumu wa yeye kuhama msimu huu.

Mkataba wake kwa sasa na wapiga nyundo hao umesalia miaka mitatu huku klabu hiyo ikiwa na chaguo la kumuongezea mwaka mmoja zaidi. (Times - subscription required)

Chelsea wana matumaini ya kumsajili mlinzi wa kifaransa Jules Kounde kutoka Sevilla huku kukielezwa kwenye mkataba wake kuna kipengele cha £77m ili kumruhusu kinda huyo mwenye umri wa miaka 22 kuhama. Vilabu hivyo viwili vilitumai beki wa Chelsea Kurt Zouma, 26, angejumuishwa kwenye mpango huo lakini aligoma kujiunga na klabu hiyo ya La liga. (90Min)

Manchester United bado inamtaka kiungo wa Rennes Eduardo Camavinga, 18, lakini inaona nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa angetamani kujiunga na Paris St-Germain au klabu ya Hispania. (ESPN)

West Ham waaangalia kama wanaweza kumsajili kiungo mfaransa wa Lille French Jonathan Bamba, 25, kama mbadala wa kiungo wa kimataifa wa England Jesse Lingard kutoka Manchester United. (Express)

Image: GETTY IMAGES

Crystal Palace wanajiandaa kutoa kitita cha £10m kwa ajili ya mshambuliaji wa Arsenal Eddie Nketiah, 22, lakini washika bunduki hao wanataka dau la angalau linalokaribia £20m. Nyota huyo anayeshikilia rekodi ya mabao kwa timu ya taifa ya England chini ya miaka 21 pia amekuwa akiwaniwa na vilabu vya Ujerumani. (Athletic - subscription required)

Kiungo wa Arsenal Lucas Torreira, 25, anakaribia kutua Fiorentina kwa mkopo baada ya kuisaidia Atletico Madrid, chini ya Diego Simeone kushinda taji la La Liga msimu uliopita alikokua anacheza kwa mkopo. (football.london)

Kiungo wa Brazil Willian, 33, yuko njiani kuondoka Arsenal bure na kujiunga na Corinthians ya nyumbani kwao, mazungumzo yako katika hatua za mwisho. (Mail)

Wolves wako tayari kutoa ofa ya £7m bid kwa ajili ya mshambuliaji wa Cardiff City na Wales Kieffer Moore,29. (Football Insider).

Image: GETTY IMAGES

Mlinzi wa Manchester United Phil Jones yuko tayari kwenda kwa mkopo kwenye klabu ya Championship, kwa sasa beki huyo muingereza mwenye umri wa miaka 29 hana uhakika wa namba Old Trafford. (Football League World)

Vilabu vya Newcastle United na West Ham vitapigana vikumbo kupata saini ya mlinzi wa kushoto wa Burnley raia wa Ivory Coast Maxwel Cornet, 24, kutoka Lyon. (90 Min)

Ofa ya Everton kwa ajili ya mshambuliaji mzaliwa wa Canada Daniel Jebbison,18 ambaye anachezea timu za taifa za vijana za England, imekataliwa na Sheffield United.

Vilabu vya Aston Villa, Brentford na Leeds vimeonyesha nia pia ya kumtaka kinda huyo. (Teamtalk)

View Comments