Image: GETTY IMAGES

Maisha ya walinda mlango wawapo golini, yanafanywa kuwa magumu na washambuliaji wakali.

Kipa wa zamani wa Real Madrid na timu ya taifa ya Hispania Iker Casillas aliwahi kusema, "maisha ya kipa siku zote yanakuwa magumu, unaokoa michomo 100, lakini watu watakumbuka mchomo mmoja tu ulioruhusu goli."

Baadhi ya washambuliaji wanafanya maisha yanakuwa magumu zaidi kwa magolikipa kutokana na uwezo wao wa kufumania nyavu. Kuanzia wakati huo Pele, Perenc Puskas, Eusebio, Alfredo di Stefano', Romario, Gard Muller, Marco Van Basten, Giuseppe Meazza, Karl-Heinz Rummenigge, George Weah, Raul, Ronaldo de Lima, Allan Shearer na Gabriel Batistuta.

Lakini makipa wengi watakutajia nyota hawa watano kama washambuliaji wanaogopeka zaidi na makipa kutokana na uwezo wa kufunga wakati wowote na kwa mazingira yoyote.

MATANGAZO

4: Zlatan Ibrahimovic

Image: GETTY IMAGES

Msweden huyu ni moto wa kuotea mbali linapokuja suala la kufunga mabao. Miongoni mwa makipa ambao hawawezi kumsahau Zlatan ni pamoja na Stephane Ruffier, ambaye alikuwa kipa wa kimataifa wa Ufaransa aliyeichezea Saint-Etienne kwa miaka 10. Alikutana na Zlatan, wakati huo, Zlatan anaichezea Paris Saint-Germain.

Mlinda mlango mwingine wa Ufaransa Steve Mandanda, ameruhusu mabao 11 ya Zlatan huku Miller aliyeruhusu mabao 9, ni miongoni mwa makipa ambao wanasimulia hatari ya Zlatan.

3: Robert Lewandowski

Image: GETTY IMAGES

Anatajwa kama mshambuliaji bora katika miaka mitatu iliyopita akifunga mabao atakavyo akiwa na Buyern Munich. Mpaka sasa alikuwa amewafunga makipa karibu 40 tofauti katika michuano mikubwa ya klabu bingwa ulaya. Sio jambo dogo

Makipa ambao wanamuhofia Lewandowski wakati wote ni pamoja na Baumann: mlinda mlango wa Hoffenheim ameruhusu mabao 16 dhidi ya Robert Lewandowski. Kipa wa Borussia Dortmund Roman Burki ni miongoni mwa makipa ambao wanamhofia sana Mpolandi huyu. Burki ameruhusu mabao 14 tangu akutane na Lewandowski kama ilivyo kwa mlinda mlango Casteels ambaye naye kapachikwa mabao 14 na Robert Lewandowski.

2: Lionel Messi

Image: GETTY IMAGES

Lionel Messi mpaka sasa ameshawafunga makipa zaidi ya 100 katika maisha yake ya soka, lakini miongoni mwa makipa waliofungwa mabao mengi zaidi na Messi ni Iker Casillas, aliyekuwa kipa namba moja wa Hispania na Real Madrid. Casillas nahodha wa zamani wa Real Madrid kafungwa mabao 18 na Messi, na usisahau Casillas ni miongoni mwa makipa bora waliowahi kucheza ligi kuu ya Hispania 'Laliga'.

Mlinda mlango wa kibrazil Diego Alves anamtambua Messi na aliwahi kukiri kuwa ni miongoni mwa washambuliaji hatari kuwahikukutana naye, Diego Alves ameruhusu mabao 21 ya kufungwa na Messi katika maisha yake ya soka.

1: Cristiano Ronaldo

Image: GETTY IMAGES

Kama unamjua mlinda mlango wa zamani wa Athletic Bilbao, Gorka Iraizoz Moreno ni miongoni mwa makipa wazuri wakongwe ambao kwenye ligi kuu ya Hispania 'La liga' walikuwa wanafanya vizuri.

Ukimuuliza Iraizoz mshambuliaji gani anamuhofia, anawataja wawili Lionel Messi and Cristiano Ronaldo. Mreno Ronaldo peke yake kamfunga mabao 15 dhidi yake, huku Javi Varas akiruhusu kufungwa mabao 13 na Ronaldo.

Kipa mwingine wa zamani wa Barcelona, Claudio Bravo, yuko kwenye orodha ya makipa wenye hofu na Ronaldo akiruhusu mabao 12 ya mreno huyo.

View Comments