In Summary
  • Xavi kuwa kocha mpya wa Barcelona
  • Klabu hiyo ya Qatar awali ilikuwa imesema kwamba mkufunzi wao mwenye umri wa miaka 41 hangeruhusiwa kuondoka
Xavi
Image: BBC

Aliyekuwa kiungo wa kati wa klabu ya Barcelona Xavi anatarajiwa kuchukua mikoba ya kuifunza klabu hiyo huku klabu anayoifunza kwa sasa Al Sadd ikikubali kumkubali kujiunga na klabu hiyo ya Uhispania.

Klabu hiyo ya Qatar awali ilikuwa imesema kwamba mkufunzi wao mwenye umri wa miaka 41 hangeruhusiwa kuondoka.

Xavi ambaye alicheza mechi 779 katika klabu ya Barcelona na kushinda mataji 25 na klabu hiyo alitumai kwenda nyumbani ili kuwa mkufunzi wa klabu hiyo na kwamba makubaliano yalikaribia kuafikiwa.

Al Sadd inasema kwamba Barcelona imelipa kifungu cha kandarasi yake ya kumuachilia.

Mshindi huyo mara mbili wa kombe la dunia na kombe la bara Yuropa akiichezea Uhispania aliondoka Barcelona na kujiunga na klabu ya Al Sadd 2015, mara ya kwanza akijiunga na klabu hiyo kama mchezaji.

Alichukua uongozi na kuwa mkufunzi mkuu baada ya kustaafu 2019 na kuwaongoza kushinda taji la ligi msimu uliopita. Klabu hiyo haijafungwa katika mechi 36 za ligi.

Klabu hiyo ya Qatar ilituma ujumbe wa twitter kwamba Xavi ni kiungo muhimu cha historia ya Al Sadd na kumtakia mafanikio katika siku za usoni.

‘’Usimamizi umekubali kuondoka kwa Xavi kujiunga na Barcelona baada ya klabu hiyo kulipa kifungu cha kumuachilia mchezaji huyo kilichopo katika kandarasi yake5’’, klabu hiyo ilichapisha katika mtandao wake wa twitter.

‘’Tumekubaliana kushirikiana na Barcelona katika siku za usoni’’.

Tangu Barcelona ilipomfuta kazi kocha wake Ronald Koeman tarehe 27 mwezi Oktoba, Xavi amekuwa akihusishwa na kurudi katika uwanja wa Nou Camp ambapo alihudumu kipindi kirefu cha muda wake kama mchezaji.

 

 

 

View Comments