In Summary

•Ronaldo alivunja simu hiyo alipokuwa akitoka nje ya uwanja baada ya timu yake kupoteza mechi dhidi ya Everton 1-0.

•Manchester United walisema wanafahamu "tukio linalodaiwa kutokea baada ya mechi ya Jumamosi Everton na klabu itashirikiana na uchunguzi wowote wa polisi".

Image: PA MEDIA

Polisi nchini Uingereza wanachunguza madai ya shambulio baada ya mshambuliaji wa Manchester United Cristiano Ronaldo kuonekana akivunja simu ya shabiki mmoja.

Picha zilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii pamoja na maoni yaliyodai kuwa alivunja simu hiyo alipokuwa akitoka nje ya uwanja baada ya timu yake kupoteza mechi dhidi ya Everton 1-0.

Ronaldo baadaye aliomba msamaha baada ya video inayomuonyesha akivunja simu ya shabiki huyo kuibuka.

Polisi wa Merseyside walisema walikuwa wakichunguza "ripoti za madai ya kushambuliwa" katika bustani ya Goodison Park siku ya Jumamosi.

"Si rahisi kukabiliana na mihemko katika nyakati ngumu kama ile inayotukabili," alisema Ronaldo akiomba radhi.

Matokeo hayo yaliharibu matumaini ya United kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa Ulaya na kukutana na timu ya Everton ambayo ilikuwa pointi moja juu ya eneo la kushushwa daraja kabla ya kuanza.

"Hata hivyo, kila mara tunapaswa kuwa na heshima, subira na kuwa mfano mwema kwa vijana wote wanaopenda mchezo huo mzuri," Mreno huyo aliongeza.

"Ningependa kuomba radhi kwa hasira yangu na, ikiwezekana, ningependa kumwalika shabiki huyu kutazama mchezo huko Old Trafford kama ishara ya mchezo wa haki na uanamichezo."

Msemaji alisema wanawasiliana na Manchester United na Everton.

Manchester United walisema wanafahamu "tukio linalodaiwa kutokea baada ya mechi ya Jumamosi Everton na klabu itashirikiana na uchunguzi wowote wa polisi".

View Comments