logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Akimbia msikitini kusali baada ya kushinda bet ya 10.5M aliyobashiri kwa Ksh 200

Kijana huyu aliyejaliwa bahati tele alikimbia kwa kasi Msikitini kwa ajili ya kutoa shukrani.

image
na Radio Jambo

Makala19 October 2022 - 10:45

Muhtasari


• Kijana huyu aliyejaliwa bahati tele alikimbia kwa kasi Msikitini kwa ajili ya kutoa shukrani kwa neema hiyo.

Kijana mmoja mpenda kandanda alifurahia sana mjini Lagos baada yake kushinda kitita cha shilingi Milioni 10.5 kutoka kwa Bet9ja aliyoicheza kwa shilingi 200 pekee.

Katika video hiyo iliyowafurahisha watu, wengi walikusanyika kusherehekea na kijana huyo ambaye hakuweza kuzuia hisia zake huku akibubujikwa na machozi tele.

Kwenye video hiyo iliyopakiwa kwenye mtandao wa Twitter ilimwonyesha kijana huyo akisali na kushukuru mwenyezi Mungu.

Baada ya kuhakikisha ushindi wake, jamaa huyu aliyejaliwa bahati tele alikimbia kwa kasi Msikitini kwa ajili ya kutoa shukrani kwa kuneemeshwa.

Umati wa watu ulimzingira wakifurahia nao wengine wakipiga vifijo na nderemo kumshabikia mshindi huyo ambaye aliingia vitabu vya kihistoria kwa watu walioshinda pesa nyingi jimbo la kwao.

Ila cha kufurahisha ni kwamba mwanamume huyo alikuwa akijishughulisha na kurudisha shukrani kwa Mungu huku watu wakipiga kelele kwa mshangao kwa pesa alizoshinda na jinsi atakavyozitumia.

Jamaa huyu alishinda wakati ambapo Liverpool waliwashinda mahasimu wao Manchester City 1-0.

Bao la Mohamed Salah dakika ya 76 lilitosha kwa Liverpool kuibamiza Manchester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza uliochezwa Jumapili, 16 Oktoba.

Huku Mohamed Salah aking’aa kwenye  EPL hivyo ndivyo kijana huyo aling’aa pia.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved