In Summary

• Kama vile nimekuwa nikifanya katika maisha yangu yote, ninajaribu kuishi na kucheza kwa heshima kwa wenzangu - Ronaldo.

Ronaldo azungumza baada ya kutemwa kukota kikosi cha Manchester United
Image: Facebook

Jumatano klabu ya Mchester United walikuwa na mchuano mkali dhidi ya timu ya Tottenham Hotspurs, mechi ambayo iliishia kwa United kuichachafya Spurs mabao mawili kwa nunge.

Katika mechi hiyo, tukio kubwa lilikuwa lile la mchezaji Christiano Ronaldo kukataa kuingia uwanjani baada ya kutakiwa kuchukua nafasi ya mchezaji mmoja aliyetolewa dakika ya 89.

Mchezaji huyo kwa hasira alionekana akikataa kuitikia wito wa kocha mkuu na badala yake akajitoma nje ya uwanja akielekea chumba cha kubadilisha nguo.

Tukio hilo lilimghadhabisha kocha mkuu pamoja pia na uongozi wa ctimu ambao Alhamisi walitoa taarifa kwa vyombo wakisema kwamba kutokana na kitendo hicho cha kuondoka uwanjani na kukataa kucheza, hatokuwa miongoni mwa kikposi kitakachochuana na Chelsea wikendi hii.

Mshambuliaji huyo matata wa timu ya taifa la Ureno amejibu taarifa hiyo ya kumfungia nje katika kikosi cha kucheza wikendi hii ambapo amesema kwamba anaheshimu uamuzi wa timu na kusema siku zote amekuwa akiweka heshima mbele dhidi ya wachezaji wenzake.

“Kama vile nimekuwa nikifanya katika maisha yangu yote, ninajaribu kuishi na kucheza kwa heshima kwa wenzangu, wapinzani wangu na makocha wangu. Hilo halijabadilika. sijabadilika. Mimi ni mtu yule yule na mtaalamu yuleyule ambaye nimekuwa kwa miaka 20 iliyopita nikicheza soka ya wasomi, na heshima imekuwa na jukumu muhimu sana katika mchakato wangu wa kufanya maamuzi,” Ronaldo alisema.

Mchezaji huyo alisema kwamba alianza kujifunza kuheshimu watu akiwa mchanga katika taaluma ya soka na alikuwa analiona hilo kutoka kwa wachezaji waliokuwa wakubwa kwake.

Pia alisema motisha aliyokuwa akiiona kutoka kwa wachezaji wakubwa kwake ndio hiyo anajaribu kuwapa wachezaji wadogo kwake katika klabu ya Manchester na kuahidi kia kitu kitakuwa sawa licha ya misukosuko inayomkumba katika timu hiyo.

“Siku zote nimejaribu kuonyesha mfano mwenyewe kwa vijana waliokua katika timu zote ambazo nimewakilisha. Kwa bahati mbaya hiyo haiwezekani kila wakati na wakati mwingine joto la wakati huu limechukua nafasi kubwa zaidi kati yetu. Hivi sasa, ninahisi tu kwamba ni lazima niendelee kufanya kazi kwa bidii katika Carrington, kusaidia wachezaji wenzangu na kuwa tayari kwa kila kitu katika mchezo wowote. Kushikwa na shinikizo sio chaguo. Haijawahi kuwa,” Ronaldo alimaliza.

View Comments