logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kwa mara ya kwanza, Tuchel azungumzia kufutwa kwake kazi Chelsea

Nilipenda kila siku katika klabu ya Chelsea. Ilifika mwisho mapema sana kwangu - Tuchel.

image
na Radio Jambo

Makala01 November 2022 - 10:32

Muhtasari


• Bado sijafanya uamuzi. Sasa ni wakati wangu wa kupumzika - Tuchel.

Thomas Tuchel amefichua mawazo yake juu ya uamuzi wa mmiliki wa timu ya Chelsea, Todd Boehly kumfuta kazi ya ukufunzi na nini mustakabali wake.

Tuchel amedai kuwa muda wake ndani ya Chelsea 'ulimalizika mapema sana' alipokuwa akiongea kuhusu kuondoka kwake kwa mara ya kwanza. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 49 alitimuliwa kufuatia kushindwa kwa The Blues na Dinamo Zagreb katika mechi ya ufunguzi wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa.

Kulingana na gazeti la The Times, Tuchel angefutwa kazi kama kocha mkuu wa Chelsea bila kujali matokeo ya Croatia. Ripoti hiyo inaeleza kuwa nia ya kumtimua Mjerumani huyo haikutokana tu na matokeo duni ya uwanjani huku kukiwa na masuala kadhaa ya nyuma ya pazia ambayo yaliwashawishi wamiliki wa Chelsea kuchukua hatua dhidi ya ukufunzi wake uliokuwa umeanza kuvurunda.

Inasemekana kuwa Tuchel hakufurahishwa na 'jukumu la ziada' na 'nguvu zaidi' katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi. Gazeti la Times liliongeza kuwa kuondoka kwa aliyekuwa mshauri wa kiufundi na utendakazi Petr Cech kulimkasirisha.

Akizungumza na Sports Star, Tuchel alivunja ukimya wake alipoondoka Chelsea mapema, akifichua kushtushwa kwake na kufukuzwa kwake. Alisema:

"Nilipenda kila siku katika klabu ya Chelsea. Ilifika mwisho mapema sana kwangu, lakini ilikuwa nje ya mikono yangu. Hili pia ndilo unalojiandikishia mkataba."

Tuchel, bila ya kustaajabisha, amekuwa akivutiwa sana na vilabu vichache ambavyo vimekuwa vikitafuta kuajiri kocha mkuu mpya. Mjerumani huyo aliripotiwa kupangwa kuchukua nafasi ya Steven Gerrard huko Aston Villa, ambapo alikataa.

Kocha huyo wa zamani wa Chelsea aliangazia mipango yake ya baadaye. Alisema:

"Bado sijafanya uamuzi. Sasa ni wakati wangu wa kupumzika. Vilabu vingine vimekuwa vikimpigia simu meneja wangu, lakini tulikubaliana kwamba hataniita hapa kwa siku hizi 18 zilizopita."


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved