logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Southampton yamtimua meneja wake mkuu Ralph Hasenhuttl

Klabu hiyo imesema inahisi kuwa sasa ni wakati mwafaka wa mabadiliko.

image
na Samuel Maina

Michezo07 November 2022 - 12:02

Muhtasari


  • •Ralph ,55, anaondoka katika klabu hiyo baada ya kuhudumu kama meneja mkuu kwa takriban miaka minne.
  • •Kutimuliwa kwa Ralph kunajiri masaa machache tu baada ya Southampton kuchapwaha 1-4 na Newcastle.

Klabu ya Southampton imemfuta kazi meneja wake mkuu Ralph Hasenhuttl  pamoja na msaidizi wake Richard Kitzbichler.

Southampton ilithibitisha kutimuliwa kwa Ralph siku ya Jumatatu na kusema inahisi kuwa sasa ni wakati mwafaka wa mabadiliko.

"Kila mtu anayehusika na klabu angependa kutoa shukrani zao za dhati kwa Ralph kwa jitihada zake zote, pamoja na kujitolea kwake bila kuyumbayumba katika muda wake wote kama meneja," taarifa ya klabu hiyo ilisoma.

Ralph ,55, anaondoka katika klabu hiyo baada ya kuhudumu kama meneja mkuu kwa takriban miaka minne.

Kocha mkuu wa kikosi cha kwanza cha klabu hiyo, Ruben Selles, atachukua usukani kutoka kwa Ralph kwa muda huku klabu ikiendelea kutafuta mridhi wa raia huyo wa Austria.

Kutimuliwa kwa Ralph kunajiri masaa machache tu baada ya Southampton kupokea kichapo cha 1-4 kutoka kwa Newcastle.

Klabu hiyo imekuwa ikiandikisha msururu wa matokeo hafifu msimu huu huku ikiwa imejizolea pointi 12 katika mechi 12 ambazo imecheza kufikia sasa.

Kwa sasa The Saints wanashikilia nafasi ya 18 kati ya klabu 20 zinazoshiriki ligi kuu ya EPL.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved