logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Neymar kukosa mechi mbili zijazo akiuguza jeraha la mguu

Alielezea jeraha lake kama "moja ya nyakati ngumu zaidi katika kazi yangu ".

image
na Radio Jambo

Makala26 November 2022 - 07:36

Muhtasari


  • Neymar aliketi huku uso wake ukiwa umefunikwa wakati alipokuwa akipata matibabu na picha zilionyesha fundo lake la mguu wa kulia likiwa limevimba

Neymar hatashiriki mechi mbili zijazo za Brazil za Kombe la Dunia baada ya kupata jeraha la mguu wa kulia, anasema daktari wa timu yao.

Mshambuliaji huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 30 aliondolewa uwanjani dakika ya 80 ya mchezo wa siku ya Alhamisi ambapo Brazil waliichapa Serbia 2-0 baada ya kukabiliwa vikali na Nikola Milenkovic.

Neymar aliketi huku uso wake ukiwa umefunikwa wakati alipokuwa akipata matibabu na picha zilionyesha fundo lake la mguu wa kulia likiwa limevimba.

Alielezea jeraha lake kama "moja ya nyakati ngumu zaidi katika kazi yangu ".

"Nimejeruhiwa, ndio sio vizuri, itaniumiza lakini nina uhakika nitakuwa na fursa ya kurejea tena kwasababu nitafanya kila liwezekanalo kuisaidia nchi yangu, timu yangu na mimi mwenyewe."

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved