Image: BBC

Waandamanaji wanaoipinga serikali nchini Iran wamekuwa wakisherehekea timu ya taifa ya kandanda kuondolewa katika michuano ya Kombe la Dunia, kufuatia kipigo chao cha bao 1-0 kutoka kwa Marekani.

Video zilizosambazwa mitandaoni zilionyesha watu wakicheza mitaani na kupiga honi za gari huko Tehran na miji mingine kadhaa Jumanne usiku.

Baadhi ya Wa Iran walikataa kuunga mkono timu yao ya soka nchini Qatar, wakiiona kama uwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu.

Vyombo vya habari vinavyohusiana na serikali vililaumu vikosi vya uhasama ndani na nje ya Iran kwa kuweka shinikizo zisizo za haki kwa wachezaji.

Wachezaji hao hawakuimba wimbo wa taifa kabla ya mchezo wao wa kwanza, kushindwa 6-2 na Uingereza, katika hali inayoonyesha mshikamano na waandamanaji.

Lakini waliimba kwenye mchezo wao dhidi ya Wales, ambapo walishinda mabao 2-0, na pia katika mchuano wao na Marekani.

Baadhi ya waandamanaji waliona huo kama usaliti kwa nia yao ingawa kulikuwa na ripoti kwamba timu hiyo ilipata shinikizo kubwa kutoka kwa mamlaka ya Iran.

View Comments