In Summary

• Gakpo amekuwa katika kiwango kizuri msimu huu, akifunga mabao tisa na kutoa asisti 12 katika mechi 14 za ligi akiwa na PSV.

• Majarida ya michezo yanasema kuwa Ada ya winga huyo inatarajiwa kuwa kati ya euro 40m-50m (£35.4m-£44.3m).

Cody Gakpo, winga wa Uholanzi
Image: Mirror

Tetesi za soka kutoka Ulaya zinadai kiuwa miamba ya Uingereza Liverpool wamefanikiwa kuzinasa huduma za mshambuliaji wa timu ya Uholanzi PSV Eindhoven Cody Gakpo.

Mchezaji huyo alifana na kutia for a pakubwa katika michuano ya kombe la dunia iliyomalizika Desemba 18 nchini Qatar japo Uholanzi waliondolewa hatua ya robo fainali ya Argentina ambao walienda mpaka kunyakua ubingwa wa dunia.

Majarida ya michezo yanasema kuwa Ada ya winga huyo inatarajiwa kuwa kati ya euro 40m-50m (£35.4m-£44.3m).

PSV wanasema Gakpo atasafiri hadi Uingereza kukamilisha dili hilo, na kuongeza kuwa huo utakuwa uhamisho wa rekodi kwao. Liverpool wamefanya uhamisho huku washambuliaji Luis Diaz na Diogo Jota wakiwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kufuatia majeraha waliyoyapata kabla ya kuanza kwa mechi za kombe la dunia.

Gakpo amekuwa katika kiwango kizuri msimu huu, akifunga mabao tisa na kutoa asisti 12 katika mechi 14 za ligi akiwa na PSV. Pia ameweza kufunga mabao matatu na kutoa pasi mbili za mabao katika mechi tano za Ligi ya Europa.

Katika Kombe la Dunia, alifunga katika kila mechi ya kundi la nchi yake dhidi ya Senegal, Ecuador na Qatar.

Liverpool wamekuwa wakisuasua mno katika safu yao ya ushambuliaji msimu huu haswa tangu kuondoka kwa mshambuliaji wa Senegal, Sadio Mane na kumsaini Gakpo kumetajwa kuwa moja ya mbinu za kujaribu kunoa safu yao ya kusaka mabao.

Gakpo akikamilisha vipimo vya afya, atatarajiwa kujumuika na wenzake Mohammed Salah, Darwin Nunez na Ferminho katika safu ya mbele kusaka mabao.

View Comments