In Summary

•Mkongwe huyo huku akijiandaa kustaafu, imeripotiwa kuwa AC Milan wamemuandalia mkataba wa ubalozi wa timu hiyo.

Ibrahimovic kustaafu mwisho wa msimu
Image: Twitter

Hatimaye imeripotiwa kuwa mshambuliaji mkongwe wa timu ya AC Milan Zlatan Ibrahimovic ametangaza kuwa huenda akafungasha virango vyake na kustaafu kutoka kucheza soka.

Zlatan amefurahia safari nzuri ya soka iliyochukua zaidi ya miaka 20, huku nyota huyo wa Uswidi akiwa na nafasi adimu ya kujiunga na vilabu kadhaa maarufu barani Ulaya.

Mchezaji huyo wa miaka 41 alidhaniwa kuwa amefika mwisho mwaka 2018 baada ya kuigura Manchester United akielekea zake Marekani kujiunga na timu LA Galaxy inayoshiriki ligi ya ya MSL Soccer nchini humo.

Lakini aliwashangaza wengi aliporudi tena katika timu ya ujana wake, AC Milan ambapo amekuwa akicheza.

Zlatan Ibrahimovic kwa sasa anapata nafuu kutokana na upasuaji wa goti aliofanyiwa majira ya joto yaliyopita na ingawa tarehe ya kurejea haijafahamika, mustakabali wake haujulikani. Kwa kweli, jukumu la balozi katika AC Milan liko tayari, ripoti inadai.

Msweden huyo alitarajiwa kurejea mwanzoni mwa 2023, nipe au chukua, na urejeshaji haujapata shida kubwa kufikia sasa. Walakini, mchakato hautaharakishwa na kwa hivyo tarehe ya kurudi haijulikani.

Kwa mujibu wa Gazzetta Dello Sport, mkongwe huyo ambaye amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya kujiradidi ambayo wengi wanahisi ni kutokana na umri kumuacha, huenda akastaafu rasmi mwishoni mwa msimu.

Jarida hilo liliripoti kuwa tayari ameshaandaliwa mkataba wa kuwa balozi wa timu hiyo baada ya kumaliza mwendo wake uwanjani salama na kuilinda Imani pamoja na kushinda vita.

 

View Comments