In Summary

• Turkaslan, 28, alichezea klabu ya daraja la pili ya Uturuki Yeni Malatyaspor mara sita baada ya kujiunga nayo mwaka 2021.

Mlinda mlango wa Uturuki Ahmet Eyup Turkaslan alifariki dunia kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea Jumatatu.
Image: Yeni Malatyaspor

Mlinda mlango wa Uturuki Ahmet Eyup Turkaslan amefariki dunia kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea Jumatatu nchini kwao, klabu yake ya Yeni Malatyaspor imethibitisha.

Waokoaji waendelea kuchimba vifusi huku idadi ya waliofariki ni zaidi ya 7,800.

"Kipa wetu, Ahmet Eyup Turkaslan, alipoteza maisha yake baada ya kukumbwa na tetemeko la ardhi. Pumzika kwa amani," klabu hiyo ilisema kwenye mtandao wake wa Twitter na kuongeza "Hatutakusahau, ni mtu mzuri".

Turkaslan, 28, alichezea klabu ya daraja la pili ya Uturuki Yeni Malatyaspor mara sita baada ya kujiunga nayo mwaka 2021.

Winga wa zamani wa Crystal Palace na Everton, Yannick Bolasie, ambaye kwa sasa anachezea timu ya daraja la pili ya Uturuki, Caykur Rizespor,nae aliandika kwenye mtandao wake wa Twitter: "RIP kaka Eyup Ahmet Turkaslan.

"Unamuoa mtu kwenye benchi la akiba sasa, baadaye unaambiwa ametutoka." Bolasie aliongeza: "Salamu zangu za rambirambi kwa familia yake yote na wachezaji wenzake wa Yeni Malatyaspor. Inasikitisha."

View Comments