In Summary

• Webb anaarifiwa kuandika barua kwa Arsenal kuomba msamaha kwa tukio lililojiri na kuona Gunners wakipoteza pointi 2 muhimu dhidi ya Brentford.

Maamuzi ya VAR kuwa hakuna bao
Image: Screengrab//Twitter

Wikendi iliyopita katika mechi za ligi kuu ya Premia nchini Uingereza, maamuzi mbalimbali ya refa yalizua mijadala mikali kwenye mitandao haswa kuhusu suala la mchezaji kuotea uwanjani.

Katika mecho ya viongozi wa ligi Arsenal dhidi ya Brentford, utata uliibuka baada ya mchezaji wa Brentford Ivan Toney kufunga bao la kichwa akionekana kuwa ameotea.

Bao hilo lilijiri baada ya vuta nikuvute kwenye lango la Arsenal wachezaji wakipukutika chini kama majani ya mti yaliyokauka na hapo ndipo Toney aliinuka juu Zaidi kuliko wote na kutua mpira wavuni.

Bao hilo ilichukua sekunde kadhaa kukubaliwa, kumlazimu refa kwenda kufuata huduma za VAR na baadae akalikubali bao licha ya wengi kuhisi halingestahili kusimama sababu ya kuotea kwa baadhi ya wachezaji.

Katika mechi nyingine pia kati ya Brighton na Cystal Palace, hali ilikuwa kama ile baada ya mchezaji wa Brighton kufunga bao lakini likafutiliwa mbali kwa kuotea licha ya kuwa lilistahili kuhesabiwa.

Kutokana na utepetevu huu wa marefa na VAR, sasa jarida la Daily Mail limeripoti kuwa mkuu wa marefa Howard Webb ameita mkutano wa dharura wa marefa kujadili matukio hayo yaliyotokea wikendi.

Mzaliwa wa Yorkshire mwenye umri wa miaka 51, ambaye alirejea Uingereza mwaka jana baada ya kukaa Marekani, amewaamuru waamuzi wote wa Ligi Kuu ya Uingereza, waamuzi wasaidizi na maafisa wa VAR kwenye mkutano siku ya Jumanne. Kuhudhuria kunadhaniwa kuwa ni lazima kwani Webb anatafuta kuzuia majanga yoyote zaidi.

Mail wanaripoti kuwa mkutano huo wa lazima unatarajiwa kuwa mkali Zaidi kwa marefa na huenda marefa na maafisa wa VAR wote waliofanya maamuzi yasiyofaa katika mitanange hiyo miwili wakamwaga unga.

View Comments